Maoni: Rais Dr. John Pombe Magufuli amefanana kiuongozi na Dr. Nkwame Nkurumah


J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
107
Likes
101
Points
45
Age
48
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined Feb 16, 2016
107 101 45
Dr. John Pombe Magufuli ni kama Dr. Nkwame Nkurumah kiutendaji.... Wewe unasemaje?

Kama alivyo JPM Dr.Nkwame alikuwa mwalimu msomi sana na alipata PhD yake kutoka University of Pennslvania sasa UPenn (One of the best Universities in the World). Kama alivyo JPM Uzalendo wa Nkurumah ulikuwa mkubwa sana, akiwa masomoni US alianza kueneza vuguvugu la ukombozi barani afrika. Wazungu hawakumpenda, na hasa Wamarekani.
Kwa Rais wetu JPM, ni mzalendo ambaye ameanzisha vuguvugu la Ukombozi wa mara ya pili kuwatoa Watanzania kutoka kwenye mikono ya Wakoloni weusi wanaosadikiwa kuwa wabaya na wakatili kuliko Wajerumani

Mwalimu Nkurumah aliondoka Ghana akiwa kijana mdogo kwenda US kusoma Chuo Kikuu cha Lincoln katika jimbo la Pennyslvania baadaya ya masomo ya miaka kumi Dr. Nkurumah aliondoka US Kwenda London UK kusoma laws na kufanya Thesis ya PhD yake. Huko London alikutana na mwanamapinduzi George Padmore Kijana Mtrinidad aliyehamia London kutoka US, kwa pamoja wakaandaa Pan African Congress kwenye mji wa Manchester 1945, hapo wakakutana na akina Marcus Garvey, Mjamaica wanamapinduzi, William Edward Burghardt Du Bois, Booker T Washingyon Wamerikani mweusi wanatema cheche ya ukombozi wakatengeneza bond na kuamua kuwa muda wa Africa kupata uhuru ni sasa na Nkurumah akatumwa arudi Gold Coast(Ghana ya sasa) kuwasaidia Africa ipate uhuru wao wakarudi makwao kuanzisha sokomoko la Usawa (civil right movement) Historia haijasema kama Mwalimu alikuwa anafahamu hii movement kwa wakati huu lakini kwa chronological events, Mwalimu alikuwa Tabora boys kabla ya kwenda Makerere.
Hawa watu walikuwa na Uchungu sana, ninapomwona Rais Magufuli akikutana na Akina Paul Kagame, rais ambaye ameamua kutengeneza nchi iliyopasuka vipande na kuifanya Rwanda ya kutamani, ni Uzalendo wa Hali ya Juu sana. Rais wetu ana uchungu mkubwa sana na wananchi wake anataka kutengeneza alliance ambayo haiwaibii wala kuchukua kutoka kwa wananchi wake bali kuongeza kwenye hazina yao na ukiangalia Paul Kagame anafanya hayo kati ya Marais wanaotuzunguka Tanzania.
Mwaka 1947, Dr. Nkurumah alifunga virago akarudi Ghana akakuta kuna vyama vya upinzani tayari, UGCC wakafanya kama CHADEMA, wakamkaribisha na kumpa ukatibu mkuu, sasa Mwenyekiti anaelimu ya Kwa baba paroko na Katibu Mkuu ana PhD mtaelewana lini? Akaanzisha harakati za Uhuru chini ya msukosuko mkubwa wa Mwingereza ambapo viongozi wote wa UGCC wakaswekwa ndani, viongozi wenzie wakasema kaa isiwe tabu wakamfukuza akahama chama na kuanzisha CPP chama kipya.
Mwaka 1950 miezi michache kabla ya uchaguzi akakamatwa akawekwa rokap lakini sauti ya Watu sauti ya Mungu uchaguzi ulipofika alipigiwa Kura akiwa gerezani kwa asilimia zaidi ya Tisini, Governor akamtoa ili aanzishe serikali akiwa Waziri Mkuu, uchaguzi uliofuata 1956 akashinda tena, na this time akatangaza Uhuru wa Ghana 1957 Marcha 6.
Uzalendo wa Nkurumah haukishia kwenye kuta za gereza zilinguruma ndani na nje ya gereza kwa sauti kubwa kuliko vipaza sauti zote nchini. kumweka ndani mpigania haki ni sawa na kumpa promo, na kumsogeza karibu na media

Baada ya Dr Nkurumah kupata Uhuru na kuwa Rais kamili, akawa na ndoto ya kuiunganisha Afrika na kuwa Rais wa kwanza wa United States of Africa. Ndoto ya Nkurumah ya kuwaunganisha waafrika ukawa mkubwa, lakini akawasahau Waghana, akaanza kutaka kuwa Rais wa Waafrika akaacha Urais wa Ghana, akaanza kutoa misaada ya Kifedha Guinea na Bukina Faso akawaacha wananchi wa Ghana wakitaabika kwa njaa.
Rais Kipenzi akaanza kupoteza imani kutoka kwa wananchi wake, na baya zaidi akaanzisha a Single Party State, akanyoosha fimbo ya Dola akaanza kuwabana wapinzani waliomkaribisha mwanzoni kwa kuwafunga magerezani na hakuna aliyesema kitu.
Kila sheria aliyotaka kupitisha ilipita Bungeni bila pingamizi, Wapinzani walifukuzwa Bungeni na kuanza kuandamwa na polisi kila kona, kesi kila mahakama, marufuku kila kitu walichotia mikononi, akawa rais kweli kweli.
Katika kipindi hiki wananchi waliendelea kutaabika. Dr. Nkurumah alikoswa kuawa mara tano katika kipindi kifupi sana. Waghana wakatamani utawala wa Wazungu, maisha yakawa magumu kupindukia, uchumi ukaharibika sana Na baya Zaidi akaamua kuchukua pesa za walipakodi Ghana akampa Rafiki yake Sekou Toure wa Guinea ili arekebishe uchumi wa nchi yake.
Alikoishia Mungu ndo anajua hata mke wake hajui. Rais wangu, usjisahau, Urais ni sawa n kuwa Mganga wa Kienyeji na Mchungaji kwa wakati moja, ikibidi unaloga, na ikibidi unawekea mikono. Wapinzani wako ni ndugu zako na zaidi ya yote wanauwezo wa kukuchonganisha na wananchi wako kirahisi sana, heri upoteze support ya watu wako wa karibu Ikulu lakini usipoteze support ya wananchi wako.
Simama katikati mkutane kati, sijui kilichotokea Ghana baada ya hapo lakini ninajchojua History has nothing to do with the Future but it give an indication of what the future is going to be. " wote tunajua siku alipopinduliwa wananchi walicheza na kunywa usiku kucha "Where did beloved son of Africa go wrong"
Lets have an open converstion my fellow Africans.

Thanks
Jipubishi
 
Ciprofloxacin.

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Messages
1,428
Likes
2,149
Points
280
Ciprofloxacin.

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2015
1,428 2,149 280
Watu wanaogopa kuko ment topic yako maana sasa hvi jela nje nje, na mimi sikoment ng'oo, tena ngoja mimi nikalale kabisa, Sina milioni 4 za faini.
 
M

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Messages
2,291
Likes
1,224
Points
280
M

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2016
2,291 1,224 280
Mbona mlisema anafanana Na Hayati baba wa Taifa?
Mbona mlisema anafanana Na Hayati Edward Sokoine?
Leo amekuwa anafanana Na Hayati Kwame Nkruma? Mwaka huu Lumumba mtasema sana Haya mie napita tu
 
Mzizi wa Mbuyu

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
5,928
Likes
1,889
Points
280
Mzizi wa Mbuyu

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
5,928 1,889 280
Hakuna kuongeza mishahara watumishi wa Umma, hakuna kupanda cheo, hakuna posho ya shs20,000 !! Lkn Wakuu wa Wilaya wasio na faida wala kazi 137 mashangingi yao, mafuta ya magari etc!! Kweli anafanya sana na Nkruma!!
 
Pastor Achachanda

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Messages
3,035
Likes
960
Points
280
Pastor Achachanda

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined May 4, 2012
3,035 960 280
Fedha nyingi zinaokolewa lakini bado maisha ni difficult sijui inakuwaje
 
cerengeti

cerengeti

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Messages
3,644
Likes
1,197
Points
280
cerengeti

cerengeti

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2011
3,644 1,197 280
Hizo ni ndoto, hawafanani na hawatafanana hata akija Yesu Kristo, ukweli utabaki palepale, John pombe magufuli atabaki kuwa John pombe magufuli na Kwame
Nkurumah atabaki kuwa Kwame Nkurumah.
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
20,776
Likes
14,983
Points
280
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
20,776 14,983 280
Una msongo wa mawazo
 
chinchilla coat

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Messages
3,702
Likes
7,233
Points
280
chinchilla coat

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined May 16, 2016
3,702 7,233 280
hahaa, maongezi yake ndio yanaonyesha hakujiandaa, maana anaongea kama mtu flani aliye paniki hivi
 
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Messages
5,669
Likes
1,696
Points
280
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2012
5,669 1,696 280
huyu rais yupo kwenye wakati mwingne kabisa.
pia ht yeye alitoa kauli kwamba urais hakutegemea kama atapata....

viongoz wa zamani walitetea ukombozi na uhuru wa mwafrika kwa namna yoyote ile hata iwe vita.

lkn viongozi wa sasa ndio hao hao vibaraka wa nchi za nje...
wanakandamiza demokrasia, uhuru wa habari wapo kujineemesha wao kwa ufisadi, utawala mbovu, wizi. ufujaji nk.
 
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
107
Likes
101
Points
45
Age
48
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined Feb 16, 2016
107 101 45
Watu wanaogopa kuko ment topic yako maana sasa hvi jela nje nje, na mimi sikoment ng'oo, tena ngoja mimi nikalale kabisa, Sina milioni 4 za faini.
Hapana naona ni uvivu wa kusoma tu sio kuogopa kukoment. Hii ni historia sio Biologia tunaongelea mambo yalipita kwa kuakisi mambo yaliyo sasa hivi.
 
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
107
Likes
101
Points
45
Age
48
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined Feb 16, 2016
107 101 45
huyu rais yupo kwenye wakati mwingne kabisa.
pia ht yeye alitoa kauli kwamba urais hakutegemea kama atapata....

viongoz wa zamani walitetea ukombozi na uhuru wa mwafrika kwa namna yoyote ile hata iwe vita.

lkn viongozi wa sasa ndio hao hao vibaraka wa nchi za nje...
wanakandamiza demokrasia, uhuru wa habari wapo kujineemesha wao kwa ufisadi, utawala mbovu, wizi. ufujaji nk.
Kugombea Urais ni jambo moja na Kuwa Rais ni jambo lingine. Historia inasemaje kwa Watawala ambao hawako tayari kushaurika. Nkurumah, aliona yeye ndo msomi pekee West Afrika, hakuwa tayari kushauriwa. Historia inatuambia nini
 
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined
Feb 16, 2016
Messages
107
Likes
101
Points
45
Age
48
J

Jipu-bishi

Senior Member
Joined Feb 16, 2016
107 101 45
Watu wanaogopa kuko ment topic yako maana sasa hvi jela nje nje, na mimi sikoment ng'oo, tena ngoja mimi nikalale kabisa, Sina milioni 4 za faini.
Hahahahahahah, sio kwamba hujui Historia, unasingizia kufungwa jela.
 
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Messages
6,920
Likes
7,526
Points
280
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined May 1, 2007
6,920 7,526 280
Mleta mada acha kabisa, Nkurumah alikuwa mwanafalsafa wa kiwango cha juu sana
 

Forum statistics

Threads 1,235,905
Members 474,863
Posts 29,239,910