Maoni na wito kuhusu tume ya bunge kuchunguza pesa za "mawasiliano" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni na wito kuhusu tume ya bunge kuchunguza pesa za "mawasiliano"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtazamaji, Aug 25, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Hi wadau

  Nina maoni, wito na mtazamo tofauti juu ya tume inayotakiwa kuchunguza na kuihauri serikali sakata la Pesa za "mawasiliano" lilioibuka katika wizara ya Nishati.

  Katika sakata Hili mhuhusika na mtuhumiwa mkuu nai Jairo na wazara ya Nishati.

  Nalipongeza bunge hasa wabunega wa upinzani na ndugu zitto kabwe kutoa hoja ya kuundwa kwa tume amabayo ikifanya kazi vizuri basi kuna matatizo yatarekebishwa na kuna makosa tunataegema hayatajirudia

  Je Tume ya wabunge itafanya kazi vizuri?
  Wasi wasi wangu na duku duku langu ni kuwa wakati kuna tatizo kubwa inaonekana wabunge na watu wengi tunaangalia sehemu tu ya tatizo. Yaani Jairo na wizaa ya Nishati. Ukweli hapa Tatizo ni serikali( Wizara) na wabunge

  CAG kishasema kitu kilichfanyika ni cha kawaida na inawezekana kinfanyika kila wizara na hata wabunge wakiwa honest wanaweza kuwa mashahidi kuwa katika bunge hili kuna wizara zimewapa pesa za "mawasiliano" ya bejeti

  Sasa Tatizo liko wapi?
  • Tatizo la kwanza ni kupoteza hela kuchunguza wizara moja kwa kitu amabcho kinafanyika kwenye wizara nyingi. Wigo na najukumu ya tume itakayoundwa yanatakiwa kwenda mbali zaidi ya wizara ya Nishati ..........
  • Tatizo lingine ni wabunge wenyewe ni wahusika na supects katika mchanganuo huu. kwa hiyo kitendo cha tume kuwa chini ya wabunge hakitatoa ukweli wote. Bunge na wabunge ni sehemu ya tatizo linalotakiwa kucngunzwa.
  So kwa mtazamo wangu bunge na wabunge kama sehemu ya tatizo haiwezi kufanya uchunguzi sahihi na makini bila kuwa impartial

  So Nini Kifanyike?


  • Naunga mkono hoja ya zitto ya kuundwa kwa tume lakini ni mapendekezo yangu tume hii iwe chini ya majaji wastaafuu na watu amabo wako nje ya mfumo wa bunge na serikali. Kwakufanya hivi bunge na wabunge watapata nafasi ya kutazmwa na kuepwa mapendekezo ya mabadiliko gani yanatakiwa kwa bunge na serikali kwa faida ya wananchi.
  • Uchunguzi wa tume huru iliydhishwa na bunge chini ya majaji wastaafu ulenge wizara zaidi ya moja na uchunguze na matumzi ya pesa za wizara mbali mbali zilizopoelekwa dodoma kipindi cha bajeti

  Nadhani wabunge wenye nia njema na nchi hasa wa upizani hawatona kitendo cha tume kuundwa nje wa abunge kama kudhalilishw abali ni kitendo cha ushindi kwa wananchi wanaowawakilisha

  Nawasilisha kwa mjadala
   
 2. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,222
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145


  Nawapendekeza hawa katika hoja yako:

  1: Jaji Warioba(aliyekuwa wazar Mkuu)
  2: Jaji Ramadhani mstaafu wa juzi juzi
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Hata mm nakubali kabisa. je hawa waheshimiwa wako tayari kukubali au wataona wamshushiwa hadhi yao ya uheshimiwa . Sijui Zitto Muanzisha hoja ile binafis ana weza uwa na mtazamo gani?

  Nimefutilia na kugoogle lile sakata la malipo ya wabunge kule UK jinsi walivyolishughulikia . Hakuna sehemu amabyo kamati ya wabunge ilikuja na mapendekezo nini kifanyike. Ilikuwa ni kamati huru nje ya mfumo wa bunge na serikali
   
 4. T

  The Engineer Member

  #4
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzamaji, wazo lako ni chanya na linaingia akilini.
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Tatizo sidhani kama kuna mbunge yeyote awe wa CCM au upinzani anaweza kukubaliana na hiyo hoja. Wengine wanaweza kuona kama ni bunge kudharauliwa.....
   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 6,905
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mi kwa upande wangu sioni hata hiyo kazi wanayokwenda kuifanya kwa kutumia hiyo tume kwa sababu kila kitu kipo wazi wanachopaswa ni kuchukua maamuzi tu hapa
   
Loading...