Uchaguzi 2020 Maoni na mtazamo wangu baada ya kuwa mjumbe katika kura za Maoni za CCM katika moja ya majimbo hapa Tanzania

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,778
28,420
Mambo pekee niliyoyabaini katika uchaguzi huu wa kura za maoni ni kama yafuatayo:-

Ni mara 100 urudi utaratibu wa zamani wa kila mwanachama wa CCM arudi kupiga kura za maoni. Huu mchakato wa sasa hivi ndio una rushwa zaidi.

Angalia wajumbe ukumbini wanakaa katika kata zao, wanakwenda kupiga kura katika kata yaani hawaachani kama pete na kidole. Hii maana yake ni kwamba ukikamata wajumbe wote katika kata 6 kwenye Jimbo la kata 20 tayari unakuwa na zaidi ya kura 180 na kwa mtu mwenye hela na ambaye ana jina kubwa ni kitu rahisi sana tofauti na zamani ambapo huwezi toa rushwa katika watu wote.

Jambo la muhimu nililojifunza ni kuwa Jamii yetu ya kitanzania bado sana katika swala la elimu hamna mwananchi anayesikililiza hoja wala sera ya mtu ndani ya ukumbi, wala hamna anayeangalia kwamba huwa unasaidia jamii yako wanachoangalia ni nani alimuona kwa shilingi ngapi, wanaingia na majina mfukoni

Ili kusaidia Vijana ndani ya chama kisiasa inahitajika kuwepo na model mpya kabisa haya mambo ya kura ya maoni ni ya hovyo, la sivyo ijulikane moja tu kwamba ukitaka kuingia katika siasa tafuta hela kwanza kisha ingia katika Siasa



1595271249028.png


1595271324190.png
 
Nafikiri utaratibu mzuri ingekuwa kila mwanachama apige kura japo yaweza kuwa gharama.lakini sasa ni wapi watafanyia kampeni wakati muko wengi ?
 
Back
Top Bottom