Maoni na Mtazamo wa Mwanasheria Alberto Msando kuhusiana na UKUTA

Activity Ratio

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
554
577
PART ONE: KUPATWA KWA JUA; DUNIA NA MWEZI TAREHE 1.09.2016; UKUTA wanasema nini? Serikali inazuia nini?

Tarehe 1.9.2016 ni siku iliyotangazwa ya maandamano nchi nzima. Maandamano hayo yana jina la 'UKUTA' na yameandaliwa na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania.
Mpaka sasa ni Chadema pekee ndio wamejitokeza hadharani kama waasisi wa 'umoja' huo. Vyama vingine vya siasa viko kimya kuhusu 'tukio' hilo. Sio tukio la kitaifa.
Ni vyema tujaribu kuangalia kilichoombwa na kilichozuiwa. Pia kuangalia sheria inasemaje kuhusu suala hili.

STAHILI (ENTITLEMENTS) ZA VYAMA VYA SIASA:

1. Sheria za Vyama vya Siasa (Political Parties Act) na za Jeshi la Polisi (Police Force and Auxiliary Services Act) zinatoa stahili ya kufanya mikutano ya hadhara (Public Meetings) na kuongozana (Processions) kwa vyama vya Siasa kwa ajili ya kujitangaza na kutafuta wanachama.

2. Pia sheria inatoa stahili ya kulindwa (Protection) na msaada (Assistance) kutoka kwa vyombo vya usalama ili kufanikisha mikutano kufanyika bila vurugu.
Kufanya mikutano ya hadhara na kuongozana Chama cha Siasa kinatakiwa kutuma taarifa (Notification) masaa 48 kabla kwa Mkuu wa Polisi wa Eneo (Police officer in charge of the area). Taarifa hiyo inatakiwa itaje jina la chama, muda na eneo, sababu za mkutano kwa ujumla au jambo lingine kama Waziri atakavyoelekeza.

Baada ya kutoa taarifa hiyo chama kinaruhusiwa kuendelea na mkutano au kuongozana ISIPOKUWA tu kama kitapokea ZUIO (Stop Order) kutoka kwa Polisi. Lazima Zuio liwe kwa maandishi na Polisi lazima itoe sababu ya kuzuia.

Polisi haruhusiwi kutoa zuio isipokuwa tu i) kuna chama kingine kimeomba kufanya mkutano au kuongozana au shughuli nyingine katika eneo hilo hilo na muda uleule ii) mkutano huo unategemewa kutumika kwa sababu ambazo ni kinyume na sheria, uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama wa raia katika eneo hilo iii) kama chama hakijasajiliwa.... Hayo ndio matakwa ya Sheria kwa ufupi.
End of Part One......

PART TWO: KUPATWA KWA JUA; DUNIA NA MWEZI TAREHE 1.09.2016; UKUTA wanasema nini? Serikali inazuia nini?

Tuanze na jina UKUTA; Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania. Je umoja huu una 'uhalali' wa kisheria? Ni umoja unaotambulika na Sheria ya Vyama vya Siasa? Je lengo lake ni kujitangaza au kupata wanachama wa chama cha siasa? SIO HALALI KISHERIA.

Tuangalie neno MAANDAMANO (Demonstrations/Protests). Je mkutano wa hadhara kujitangaza au kupata wanachama ni kitu kile kile na maandamano ya kupinga Udikteta? Walichoomba Chadema kufanya tarehe moja ni nini kwa mujibu wa Sheria? WANACHOOMBA SIO WANACHOTAKA KUFANYA.

Lakini pia tuangalie ZUIO LA RAISI: Raisi amepiga marufuku mikutano ya kisiasa iwe ya hadhara au ya ndani. Polisi ndio wanaozuia. Je Raisi anayo mamlaka kutoa zuio hilo? HANA MAMLAKA. Pia maagizo ya Raisi sio ya kutolewa kwa mdomo!! Mwenye mamlaka ya kuzuia ni Polisi.

NINI KIFANYIKE?: Sheria inatoa nafasi kwa mtu ambaye amezuiwa na Polisi (kwa Stop Order) kukata rufaa kwa Waziri husika. Uamuzi wa Waziri ni wa mwisho. Kukata rufaa hakutakuwa na matokeo tofauti. Waziri hawezi kwenda kinyume na Raisi wake. HAIWEZEKANI.

Je, Mahakama inahitaji kutoa tafsiri? Sidhani kama kuna kisichoeleweka kwa pande zote mbili. Kuna uwezekano wa 'maamuzi ya pamoja' ya kutokuelewa. Mahakama itatumika aidha kubariki kutokuelewa kwa upande mmoja wapo au kulichanganya suala hili la kisiasa na sheria.

Chadema wanatakiwa kuachana na 'maandamano'. Jina walilochagua na "nia yao njema" haviendani! Wasitegemee huruma ya wananchi. Kulazimisha UKUTA kuendelea ni kukaribisha mvurugano kati ya polisi na wafuasi wao. Hiyo itakuwa ni tafsiri ya uvunjifu wa amani ambayo polisi watatumia!! Na uvunjifu wa amani ni kichaka kikubwa sana kujificha!

Serikali itafakari upya. Raisi asikilize ushauri. Yeye atekeleze ahadi na aachane na siasa za wapinzani. Hana sababu ya kuogopa vivuli. Yeye na chama chake wana deni la maendeleo kwa wananchi. Makatazo yake ndio chanzo cha 'maandamano' ya kumpinga. Kukataa kuwasikiliza wapinzani na kuendelea kuamini kwamba yuko SAHIHI kwa sababu ni Raisi anakosea. Hili ni tatizo la KUJITOA UFAHAMU Raisi; Chadema na Polisi Wanajua.

PART THREE: KUPATWA KWA JUA; DUNIA NA MWEZI TAREHE 1.09.2016; UKUTA wanasema nini? Serikali inazuia nini?

Hili ni tatizo la KUJITOA UFAHAMU Raisi, Chadema na Polisi. Wote wanajua na wanaelewa sheria inasemaje, wana stahili/haki zipi na kwa utaratibu gani!

Ushauri wangu wananchi wakae majumbani. Hao watatu wakutane barabarani katika kupatwa kwao. Tutatoa pole na kuchangia damu. Kwenye giza tutabaki.

AGM 2016' *JUA=RAISI, DUNIA=CHADEMA na MWEZI=POLISI.
 
kauli ya viongozi wa Chadema ni sheria. Hua hakuna nafasi ya tafakari kwa wanachama. Kufanya maamuzi binafsi ni kosa la jinai chadema.

Unaamini rais yupo sawa? kwa muktadha upi
 
Wasomi wetu ni majanga sana, anashindwa kuona hatari ya kukandamiza na kutofuatwa KATIBA ya nchi???

Anashindwa kutambua lengo la 'ukuta' ni ku uphold katiba yetu???

Anashindwa kutambua kwamba constitutional law retains supremacy against any law of the country???
 
Wasomi wetu ni majanga sana, anashindwa kuona hatari ya kukandamiza na kutofuatwa KATIBA ya nchi???
Anashindwa kutambua lengo la 'ukuta' ni ku uphold katiba yetu???
Anashindwa kutambua kwamba constitutional law retains supremacy against any law of the country???
Kwa hiyo unamshauri akaungane na yule profesa aliyeukataa uenyekiti na alivyoamrishwa na waliomtuma anautaka tena!
 
Msando asibezwe ana hoja ya msingi,

ukuta haijasajiriwa hivyo haitambuliki kisheria,

waondoe neno ukuta nadhani kwa maoni yake serikali inaweza ufikiria upya uamuzi wa kupiga marufuku.
Siddhani kama kuna ukweli.

Msando fafanua upya.
 
Anashindwaje kuelewa kuhusiana na uhalali? Umeshindwaje kutofutisha operation na chama? Ukuta ni operation ya kupinga udikteta kwa maelezo ya waasisi wake, je inatambulika kwenye sheria za vyama vya siasa? Itatambulikaje na wakati sio chama cha siasa ni operation? Swali hapo lingekuwa kama ni halali kufanya operation na jibu ni ruhusa ila wasivunje sheria.
 
Polisi ni watanzania,chadema ni watanzania wanaukuta ni watanzania tuna wajibu wa kuangalia njia bora ya kumaliza sintofahamu hii badala ya kuona fahari kushindana nwisho wa siku sisi bado ni watanzania wale wale
 
Back
Top Bottom