Maoni: Msako makali ufanyike kubaini wahudumu wa afya wanaotumia vyeti bandia nchini.

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,783
2,000
Wapo wanaodhani kuwa sekta ya ualimu ndio inayoongiza kwa kuwa na watu wanaotumia vyeti feki, lakini Mimi kwa upande wangu naona sekta ya afya ndio inayoongoza kwa sasa katika suala hili.
Jana tumeshudia ukamataji wa shehena za vyeti bandia, mitambo na watu wanaojihusisha na utengenezaji Wa vyeti hivyo huko mkoani Kigoma. vyeti hivi kwa kiasi kikubwa vinahusu sekta ya Afya, na suala hili la watu kutengenezewa vyeti feki kwa mkoa Wa Kigoma limeshazoeleka kwani limenza tangu miaka ya 2000, sijui kwa mikoa mingine.
Suala hili huenda sambamba kabisa kwa ushirikiano na watumishi wakubwa Wa sekta ya afya waliopo serikalini ambao husaidia kuwezesha baadhi ya mikakati.

kwa mfano MTU aliyemaliza darasa la saba/kidato cha NNE anaweza kwenda kwa jamaa mwenye duka la dawa au maabara akamfundisha namna ya kugawa dawa au kupima baada ya miezi mitatu/ sita MTU huyu anakuwa tayari ana kaufahamu juu ya kazi hii ambapo suala linalofuata ni kutafutiwa cheti bandia. vyeti hivi vinakuwa na sahihi za watu wanaotambulika na vingi huonekana vimetolewa Maweni, Mlimani, Kabanga na hata Bugando

kwa kupitia huu mchezo hatari, wapo watu tangu mwaka juzi wamefanya Mishe na hatimaye kuingizwa serikalini. unaweza usiamini lakini ukweli ndio huo. mkakati huu unasukwa na mtandao Wa watu wengi ambao hushirikiana na watumishi walioko serikalini na unachopaswa kufanya wewe ni kutoa si chini ya mil ili kukamilisha mchakato mzima Wa kuingizwa seriakalini, na kweli mchakato unaisha.

huku ni kucheza na afya za watu hivyo nashauri serikali kufanya msako makali katika zahanati, vituo vya afya na mahospitali kuwabaini watu Wa aina hii na kuwaondoa kwani wapo .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom