Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
MKIJA KUNIPEKUA MSISAHAU NA BARUA YA KUNIITA KAZINI
Na Rashid Chilumba
Mimi nipo nyumbani, Muda wote, siondoki wala siogopi. Nasubiri, tena nasubiri kwa shauku hiyo operesheni ya kuwatafuta tusio na kazi.
Japo hadi sasa sielewi nikishakaguliwa nini kitafuata, ila mimi nasema njooni tu mtanikuta, maana sina pa kwenda nipo tu nyumbani kutwa, nikishagombea vitumbua na watoto asubuhi nasubiri ugali wa mchana. Nifanyaje sasa?
Siko Peke yangu, niko na wenzangu, tupo wengi, njooni, sote kula kulala, ikiwa Kuna kutukamata mkigundua hatuna cha kufanya nawasihi mkodi mabasi yote ya mwendokasi ndiyo tutatosha.
Mie nina kalabrasha la kila aina ya cheti hakuna wa kunizidi, ninacho cha shule ya msingi, sekondari ya chini na ya juu, kipo cha shahada ya Kwanza tena ya heshima nikisomea Sosholojia, nlipomalizana na visa vya SUP na CARRY nkajua nimemaliza, asalaleeee…..
Nkazungusha kote vyeti sina nlipoambulia, nkaona labda haifai sosholojia, nikaenda kujifunza udereva, kisha kuongoza watalii, hakuna hata dala dala iliyokosa dereva wala kampuni ya utalii ilo na nafasi. Mlitaka nifanyaje?
Kila sehemu nikienda niwe nimefanya kazi walau miaka 3 kama uzoefu hahahaha hahahaha kichekesho, nimefanya lini ndo nimetoka kufunzwa?
Zile asilimia tano za halmshauri nlizoambiwa zipo sijui anapewa nani maana kila ninayemjua hakuna alowahi kupata, maana nlishawaza kufuga Kuku na kulima ufuta, sasa sina senti, mlitaka niibe?
Halafu nyie badala ya kutufanya tuwe kazini mnakuja kutukagua na kutukamata? Hamjui wenzenu huko duniani wanafanyaje au mzuka tu na amri zisokwisha?
Kwanza lazima ieleweke vijana kukosa ajira ni jambo la dunia nzima, hakuna asiyetaka kazi ili ale na kuvaa anachotaka au asaidie wengine.
Hata wewe Mtoa amri, isingekuwa siasa pengine hukuwa na sifa za kuajirika kwenye soko.
Nani anapenda kuchakaza viwalo vyake juu ya kochi au kumsikiliza Diamond kutwa kucha kwa kuwa hana cha kufanya? Hayupo
Sasa wenzenu duniani hawawasaki watu bali wanatengeneza mazingira ya kuwaingiza kazini, wanafanyaje?
#Mosi, Wanashawishi kampuni na taasisi kuondoa Muda mrefu wa uzoefu kwa waajiriwa wapya katika kazi za wafanyakazi wa kawaida (Junior officers),
ni ajabu mtu ametoka chuoni halafu atakiwe kuwa amefanya kazi miaka miwili au mitatu ndiyo aajiriwe, sasa uongozi wa kieneo kama Jiji au Mkoa unaomba makampuni katika eneo hilo kupunguza urefu wa Muda wa uzoefu, hivyo watu wengi wanaingia kazini haraka.
#Pili Viongozi wanaandaa makutano ya kivitendo kila msimu wa likizo kwa vijana katika eneo lao. (Youth Inspirational Camps)
Ndo utasikia vitu kama Summer Camp huko ulaya, vijana wa kada tofauti hukutana sehemu moja wakati wa likizo na kupewa mafunzo ya vitendo na makampuni makubwa.
#Tatu Viongozi huratibu mfumo wa taarifa wa kuarifu watu wake taaluma inayopendelewa zaidi sokoni na yenye ajira nyingi.
Hapa nyumbani kila mtu anasoma anachosikia kwa mwingine sio kwa taarifa rasmi kwa eneo hilo ndio lina uhitaji mkubwa wa wafanyakazi, mtu kazaliwa Nachingwea na akimaliza anarudi Nachingwea ila anakwenda kusoma usanifu Majengo. Huko hadi leo fundi ndo mkandarasi utamchorea nani jengo?
#Nne Viongozi wa kieneo wanahakikisha mitaji ya fedha na rasilimali nyinginezo zinapatikana kuwasaidia vijana.
Meya wa Kinondoni ni mfano, vikundi vya vijana vinaanzishwa na kupewa hamasa kwa kupewa fedha, kusaidiwa mafunzo n.k sio mikwara ya kuwakamata.
Miradi ya kilimo, ufugaji na kutoa huduma inaanzishwa. Huku Street wengi hatujui lolote kuhusu asilimia tano za halmshauri, hakuna majarida wala mabandiko watu wanazipiga tu
#Tano Viongozi wa kieneo wananyakua fursa kutoka serikali kuu na kuishusha kwao.
Wenzetu viongozi wa kieneo kama mameya wanashindana kuleta fedha Za serikali kuu kwao. Kwa mfano RC Makonda angeweza kwenda kwa Rais na kujieleza kuwa mradi wa kutengeneza madawati wapewe vijana wa Dar badala ya Jeshi, kisha Una Mobilize haraka haraka timu yako inapata pesa mnatengeneza madawati.
#Sita Uwekezaji kwenye sekta ya Ujenzi na viwanda .
Kwa kuwa sio vijana wote wana Elimu ya kuajirika kisekta uwekezaji kwenye ujenzi na viwanda kunasaidia kuwaingiza vijana wasio na Elimu kubwa katika ajira. Maana sekta hizi hazihitaji akili sana bali nguvu na ujasiri.
Hivyo kwa kuwa hayo mlikuwa hamuyajui bali mlikuwa mnawaza kutupekua tu ndiyo nasema Mkija kunipekua msisahau barua ya kuitwa kwangu kazini, nitaanza hata kesho.