Maoni: Misingi ya Usalama wa Taifa. Sizungumzii TISS

selemala

JF-Expert Member
Feb 14, 2007
367
245
Tunapoongelea Taifa, inatakiwa iwe MWIKO kuachia maamuzi yoyote ya kitaifa yafanywe na mtu mmoja au kikundi kimoja cha watu, bila kuwa na vikundi vingine huru (kiufanyaji kazi) vyenye jukumu la kuyapima maamuzi hayo na kuwa na uwezo wa kuyatengua yanapothibitika kuwa hayana faida, yanavunja sheria za haki na usawa, ni hatarishi, n.k. kwa Taifa.

Kwangu mimi muundo huu ndio msingi thabiti wa Usalama wa Taifa (kwa maana halisi ya maneno haya na sio kwa maana ya TISS).

Ninafikiri
, kama hatutakuwa na muundo wa mfumo wa utawala wenye kufuata dhana hii, basi siku za kuwa na Tanzania/Tanganyika kama Taifa moja huru zinahesabika.

Moja ya njia za kutekeleza muundo huu ni kuwa na Serikali , Bunge na Mahakama HURU zilizo sawa kimamlaka, kila moja yenye jukumu la kumdhibiti mwenzake (ukiachana na majukumu mengine).

Na iwapo vyombo hivi vitatu vikishirikiana kuhujumu nchi, basi iwe ni Haki ya msingi kwa wananchi (Wenye nchi) kufanya lolote linalohitajika kuvivunja vyombo hivyo na kuunda vingine haraka iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom