Maoni: Mikutano ya siasa ifunguliwe kipindi hiki cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Wanabodi umofia kwenu

Nianze kwa kumpa pole na hongera Mh. Rais Magufuli kazi njema anazofanya kila siku,

Hoja yangu ni alipokuwa anaingia Madarakani alipiga marufuku mikutano ya kisiasa na kusema tufanye kazi siasa itakuwa kipindi cha uchaguzi.

Sasa tupo katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa naomba kupendekeza mikutano iruhusiwe ili kuleta demokrasia kwa wote.

Nyinyi mnaomsaidia Rais Magufuli mkumbusheni wakati ndo huu

Swali je kuna uchaguzi usio na kampeni hapa Tanzania?

Nni maoni yako?
Naomba kuwasilisha.
 
Washindi wanajulikana haina haja mzee baba analijua hili,kwakua ni katiba vinginevyo ningeshauri uchaguzi wowote usifanyike kuanzia serikali za mitaa mpaka Urais hadi 2025 viongozi wabaki wale wale maana tunapoteza muda na fedha.
 
Back
Top Bottom