Maoni mbalimbali ya wanasiasa juu ya Lawrence Masha kujivua uanachama wa CHADEMA

NIMEPENDA FIKRA PEVU ZILIZOTOLEWA HAPA,KWELI CHADEMA WAMEKOMAA KI FIKRA,
NI HAKI YAKE / NA NDIO UHURU SAHIHI NA DEMOKRASIA ILIYOPO NDANI YA CDM,AMETUMIA HAKI YAKE YA KIMSINGI KABISA,MAAMUZI YAKE YAHESHIMIWE,NANYI UPANDE WA PILI IGENI HAYA,KWANI YOTE NI KWA USTAWI WA JAMII NA TAIFA, KUHAMA CHAMA SIO DHAMBI.
 
MANGE KIMAMBI AMESEMA;

"Masha amenipa taarifa nyingi sana za kumchafua JPM na Bashite. Na alikua akinikumbusha nipost. Amenipigia simu na kuniandikia text nyingi sana za kumchafua JPM na Bashite. Mwambieni abishe niweke voice note na screenshot zote. Nimetunza ushahidi" Mange Kimambi 15/11/2017.

C&P
 
MANGE KIMAMBI AMESEMA;

"Masha amenipa taarifa nyingi sana za kumchafua JPM na Bashite. Na alikua akinikumbusha nipost. Amenipigia simu na kuniandikia text nyingi sana za kumchafua JPM na Bashite. Mwambieni abishe niweke voice note na screenshot zote. Nimetunza ushahidi" Mange Kimambi 15/11/2017.

C&P
Mwambieni Mange awataje na Nyumbu wengine wanaompelekea taarifa, maana kashaonyesha mwelekeo wa kundi lake...
 
Demokrasia imechukua mkondo wake. Ila CDM watupe mikakati ya kuchukua dola 2020! Hii kujenga ofisi za chama mbona haipewi kipau mbele? Iundwe kikosi maalumu ndani ya chama kushughulikia ujenzi wa ofisi za chama za mikoa na wilaya.
 
mmmh we mdada,utamuaribia mwezio.Kaona upepo hauvumi vizuri kwa Ukawa kala kona.
 
Masha hakumia rasilimali ila nyalandu muda si mrefu ataukwaa tayari alishaanza kutumia rasilimali nairobi!

Breaking news,kuna mwelekeo mzuri Zimbabwe,.Zimbabwe jeshi limeanza kazi,wale waliokuwa wamemzunguka Mugabe wahuni wa umoja vijana Zanu pf /uvccm ,wakishirikiana na Grace,wameanza kudhibitiwa ,walisema watapigana kufa,milio ya risasi ilisikikana,jeshi limedhibiti ikulu,habari,Munangangwa yupo johanesburg anarudi kuja kuchukua umakamu wake,akiungwa mkono na jeshi,tunaomba amani,heshima na democracy iliyopotea irudi,yaliyokuwa yanatokea zimbabwe yanafanana na hapa,tunawauliza wazee wakongwe,wakombozi halisia wa nchi hii,wako wapi,nchi imekosa mwelekeo hii,haki za binaadamu zinavunjwa,uchumi uliojengw- Miaka na wakongwe waliopita unaharibiwa,kuna kundi dogo la kihuni,linaiburuza nchi vibaya sana katika historia ya nchi hii, ikiendelea kwenda hivi,kuna ????????.
 
Kwa maoni yangu Maisha nje ya CCM hasa kwa wale waliokwisha kuonja utamu wa maisha ndani ya CCM ni mateso na mzigo mzito. Sasa mtu ameingia ndani ya chama cha upinzani miaka miwili tu anaota kushika dola. Chama kina zaidi ya miaka 20, hebu fikiri hao aliowakuta wakijenga chama wangekata tamaa ndani ya miaka miwili ingekuwaje? Ni kweli sababu za kujitoa alizozitoa Masha ni dhaifu na haziendani na hadhi yake kielimu na kiuzoefu. Ni bora awe wazi tu ya kitu chema kilicho mbele yake alichoahidiwa na hao jamaa. Unajua ndani ya chama tawala kuna fursa nyingi sana! Hivyo wale wote wanaofikiri kuhama chama tawala wajue kabisa wanaingia katika ulimwengu wa mateso, kukosa kazi, kunyanyaswa, kuharibiwa mali, kupigwa risasi na wasiojulikana na mengine mengi. Na kama wewe ni mtenda maovu na upo ndani ya CCM usijaribu kutoka, kaa humohumo ili uendelee kuwa salama, maana siku unatoka tu utaitwa mwizi, fisadi, n.k. Kwa maana nyingine asilimia kubwa kama siyo wote ndani ya chama tawala ni waovu, wezi, wapiga dili, n.k. hebu wewe fikiri mtu anahama chama tawala leo halafu kesho anaambiwa ni fisadi mkubwa, Swali linakuja kwanini wamesubiri hadi ahame chama ndipo wamtuhumu? Ina maana hicho chama ni kiwanda cha kuzalisha wahalifu.

Watanzania tunapenda upinzani uendelee kuwepo ili kusukuma maendeleo mbele na kuifanya serikali isilale usingizi.
 
Tuweke akiba ya maneno, Lowassa atakapoimiliki Chadema kwa 100% Masha atarejea ni swala la muda tu!
CHADEMA ni chama cha watu siyo kama chama kile ambacho mmebaki na minung'guniko mioyoni huku mkiwa kwenye maumivu makali kwa katiba yenu mbovu
 
Tunawaambia kila siku
Tanzania hakuna Upinzani kuna Wasaka Tonge tu!

Na Mwenye kufikiria Vizuri Cdm sio chama chakuiongoza nchi hii never
Akili ndogo Kuongoza Akili kubwa Ni Moja ya maajabu yaliyopo Cdm
 
Back
Top Bottom