Maoni: Mama Maria Nyerere apumzishwe na matukio ya kiserikali, atulie ailinde afya yake

Wakuu nawasalimu kwa jina la muumba wetu sote.
Nimejaribu kuwaza tu kuhusu umri wa mama Maria Nyerere na haya matukio ya kiserikali tukizingatia na hali ya hewa ya huu ulimwengu kwa sasa naona ingekuwa vema tu kukampumzisha maana ni hafla ashahudhuria nyingi mno, kwa sasa anastahili kutulia kijijini Butiama na kulinda afya yake huku akimshukuru muumba wake kwa umri maana nao si kidogo.
Tunaotaka ushiriki wake au kumwona tumfuate nyumbani kwake.
Note: "Usirithi adui wa mtu, tengeneza adui yako mwenyewe" - JKikwete.
Kwani Maria Nyerere anakwenda kwa hiari yake? Anatekwa na UVCCM na akijifanya mbishi anaweza kubambikiwa kesi ya ugaidi!
 
Sawa mkuu....

Ila kuna mtu wa kumlazimisha mama Maria Nyerere kwenda katika dhifa Kama hizo?!!

Kwanini tusifikiri kuwa yeye mwenyewe anapenda kutokea katika hizo dhifa....na leo ni kumbukizi ya mumewe hayati Mwalimu JKN.....

Familia ile ina watu wengi weledi mno....mno....mno....yaani akina mzee Butiku wamlazimishe mama Maria?!!

Mzee Mwinyi hajui kama anaishi Dar na hii nchi ni Tanzania sembuse huyu mama?
 
Nadhani Waandaazi wa hizi shughuli ni Watu wazima na wenye weledi..Sidhani kama akisema leo sijisikii vizuri watamlazimisha.

Huenda hata yeye anafurahi kuona Wajukuu, sio kila Mtu hupenda kukaa tu mahali pamoja muda wote.
 
Mkuu unataka kuniambia anatuma request mwenyewe kupitia watu wake wa familia?..maana huwezi kukaa meza kuu tu alipo Rais kirahisi tu kama hujapangwa kuwepo pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana ni kweli anaalikwa....je Ni lazima kwenda katika mwaliko?!!

Ni Mara ngapi humuoni Mzee wetu Salim Ahmed Salim katika dhifa tofauti...kwani haalikwi?!!!
 
Watu wanatafuta political milage kaka, hilo la kusema bibi anahitaji kulala hawajali.
 
Inawezekana ni kweli anaalikwa....je Ni lazima kwenda katika mwaliko?!!

Ni Mara ngapi humuoni Mzee wetu Salim Ahmed Salim katika dhifa tofauti...kwani haalikwi?!!!
Kwa hiyo mnategemea bibi atumie logic yake kuamua kwenda kwenye mwaliko au kutokwenda?
 
Huenda hoja Yako Ina maana!

FB_IMG_1634260818781.jpg
 
Back
Top Bottom