Maoni: Mama Maria Nyerere apumzishwe na matukio ya kiserikali, atulie ailinde afya yake

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,112
2,379
Wakuu nawasalimu kwa jina la muumba wetu sote.

Nimejaribu kuwaza tu kuhusu umri wa mama Maria Nyerere na haya matukio ya kiserikali tukizingatia na hali ya hewa ya huu ulimwengu kwa sasa naona ingekuwa vema tu kukampumzisha maana ni hafla ashahudhuria nyingi mno, kwa sasa anastahili kutulia kijijini Butiama na kulinda afya yake huku akimshukuru muumba wake kwa umri maana nao si kidogo.

Tunaotaka ushiriki wake au kumwona tumfuate nyumbani kwake.

Note: "Usirithi adui wa mtu, tengeneza adui yako mwenyewe" - JKikwete.
 
Sijui kwanini viongozi wetu wa nyakati hizi wanapenda maonyesho sana!

Ni kwa sababu hawana hoja wala agenda.

Hawana mvuto wala ushawishi.

Uongozi wao ni kwa mujibu wa hadaa, wizi na udhulumati hadi wa maisha ya watu.

Hawautumikii umma bali matumbo yao na familia zao.

Hawana nia ya kutoka madarakani bali kurithisha watoto na jamaa zao madaraka.

Mengine ni usanii tu.

Cc: Jumbe Brown, Ezekiel Mbaga BAK
 
Wenzako wanakula pesa kupitia huyo mama. Umesahau hadi kwenye kampeni za Magufuli walimbeba. CCM ni ukoo wa fisi. Tena akifa ndio yatafurahi kweli ili yautembeze mwili Tanzania nzima yapige hela.
cc Majaliwa na Jenistee Muhagama.

Hawa ndiyo wanaojenga ofisi ya mtu mmoja ya 19bn/-

Ndiyo wenye kutuaminisha rais katoa hela zake mfukoni

Ndiyo wenye kupalilia mgawanyiko wa watu na kuwa leo tuna magaidi

Kwa hakika Nyerere angerudi bakora zingewahusu sana:

Askofu Niwemugizi: Nyerere angekuwapo angewacharaza CCM viboko
 
JamiiForums-460750266.jpeg
 
Ni kwa sababu hawana hoja wala agenda.

Hawana mvuto wala ushawishi.

Uongozi wao ni kwa mujibu wa hadaa, wizi na udhulumati hadi wa maisha ya watu.

Hawautumikii umma bali matumbo yao na familia zao.

Hawana nia ya kutoka madarakani bali kurithisha watoto na jamaa zao madaraka.

Mengine ni usanii tu.

Cc: Jumbe Brown, Ezekiel Mbaga BAK
🤣🤣
Kwa hiyo ili waonekane wana hoja na agenda ni kwenda kufanya maadhimisho katika kaburi la Mwalimu Nyerere?!!!

Kwani Leo ndio mara ya kwanza kuwa kumbukizi ya baba wa taifa?!!!

Nakukumbusha tu mh.Rais ameshatangaza mwakani mwenge wa Uhuru utazimiwa Kagera na si tena Chato komredi......
 
Mkuu mbona kujishtukia?

Mada iliyopo hapa inamhusu mama Maria kupumzishwa.

Mikusanyiko ya watu kwenye zama hizi ni hatari kwa afya yake.

Unadhani fikira hizi hazina mashiko?
 
Mkuu mbona kujishtukia?

Mada iliyopo hapa inamhusu mama Maria kupumzishwa.

Mikusanyiko ya watu kwenye zama hizi ni hatari kwa afya yake.

Unadhani fikira hizi hazina mashiko?
Sawa mkuu....

Ila kuna mtu wa kumlazimisha mama Maria Nyerere kwenda katika dhifa Kama hizo?!!

Kwanini tusifikiri kuwa yeye mwenyewe anapenda kutokea katika hizo dhifa....na leo ni kumbukizi ya mumewe hayati Mwalimu JKN.....

Familia ile ina watu wengi weledi mno....mno....mno....yaani akina mzee Butiku wamlazimishe mama Maria?!!
 
Back
Top Bottom