Elections 2010 Maoni kwa wana JF

Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
533
225
Ni kweli yawezakua hawa mafisadi walifanya uchakachuaji wa kura za uraisi.
Lakini hata hivyo kulingana na vyama vya upinzani kutokua na umoja na nguvu ya pamoja hawakuweza kufika hadi vijijini kuelemisha wapiga kura sawa sawa. Hata Dr Slaa nakumbuka alikiri siku akihojiwa na waandishi wa habari wakati alipohitimisha kampeni zake. Pia ukiangalia majimbo mengi waliyoshinda vyama vya upinzani ni yale yaliyo mijini kwa sababu waliweza kufika na kuelemisha wapiga kura vizuri.
Sasa basi hata kama kura za uraisi zisingechakachuliwa ni dhahiri bado JK angeshinda kutokana na chama chake kua na mtandao mpaka vijijini.
MAONI YANGU ni kwamba Dr Slaa ni mpambanaji mzuri na ameongeza nguvu mpya katika siasa za Tanzania lakini kwa sasa tunaomba akubali matokeo na ahudhurie sherehe zote za uapishaji ili vijana wake waweze kwenda kufanya kazi tuliyowatuma kwa amani.
Bila Raisi kuapishwa hakuna serikali,...na kama hakuna serikali bunge pia halipo.
TANZANIA NI MOJA HAKUNA UKABILA WALA UDINI WALA UCHAMA....ila kuna ufisadi.
KILA LA KHERI MH SLAA 2015.
 

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,310
2,000
TANZANIA NI MOJA HAKUNA UKABILA WALA UDINI WALA UCHAMA....ila kuna ufisadi.
KILA LA KHERI MH SLAA 2015


thanks
 

3D.

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,014
1,500
tanzania ni moja hakuna ukabila wala udini wala uchama....ila kuna ufisadi.
Kila la kheri mh slaa 2015


thanks

preta unadanganya. Si kweli kuwa tanzania hakuna udini? Unajua jinsi waislamu wanavyolalamikia kunyanyaswa? Unajua kuwa gazeti la al-huda na annuur yamekuwa mstari wa mbele kumtusi dr slaa kuwa ni padri, papa na aliyechochea mauaji ya mwembechai?

Haujui kuwa lowassa alishiriki ufisadi richmond lakini katetewa kwa kuwa ni ccm? Unajua report ya "serious froud office" juu ya chenge lakini ndiye anagombea uspika sasa? Huu si u-ccm?

Natambua penye vita na mifarakano akina mama na wanawake ndo huathirika zaidi lakini hii isiwe sababu ya kuudanganya umma kuwa hakuna ukabila.

Tafuta njia nzuri ya kusisitiza amani lakini si kwa kudanganya.

Hongera kwa avatar mpya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom