Maoni kwa Tume na Taifa kwa Chaguzi Kuu zijazo mbali na wa 2015

Barya

JF-Expert Member
May 5, 2012
950
1,190
Kupitia uchaguzi huu na Kampen zake kuna makosa kadhaa tumegundua yapo na yatahitaji kurekebishwa hapo baadae, Ili hapa pia hata msajili wa vyama vya Siasa.

Namnukuu "YAPO MAPUNGUFU MADOGO LAKINI YASISABABISHE TUKALETA VURUGU NCHINI" Ina maanisha kwamba yapo mapungufu katika mchakato mzima wa uchaguzi huu, na mtu anaposhindwa uchaguz inakuwa miongoni mwa kisingizio atakachotumia, hvo tume ihakikishe inafanya haya.

1. Iajiri wafanyakazi wengi wa kudumu ili kupunguza presha za kurekebisha daftari la wapiga kura kila uchaguzi mkuu, hao wawe na jukumu la kuboresha daftari kila muda na wale kiapo cha kufanya kwa weledi kabisa kabisa.

2. Tume iwe na chanzo cha habari na mbinu ya kuwa inatoa fursa kuongea na wananchi kila mara, na kutoa taharifa sahihi.

3. Afya ya wagombea, kiwepo kipengele cha kumtaka mgombea kuthibitisha utimamu wa akili, afya ya kawaida, hii itaepusha kuja kupata kiongozi ambaye anarukwa na akili, au ambaye afya yake ni dhaifu sana.

WEWE MSOMAJI UNAHISI KINGINE NI NINI?
 
Back
Top Bottom