GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,099
Wanabodi, Napandisha huu uzi nikiomba hoja zangu zijibiwe na Bank of Tanzania au mtu yeyote ambaye amepractise Banking pande zote mbili upande wa kuendesha Bank za Biashara mfano Exim, CRDB, DTB, I AND M Bank na zingine nyingi tulizonazo Tanzanian, na Upande wa pili ni upande wa Supervision hapa naoengelea hawa wanaojiita Regulator au wasimamizi yaani Benki kuu
Mosi : kushusha rate kutoka 9 percent mpaka 7 percent ili Benki ziweze kuchukua pesa toka BoT na zianze kukopesha, Je watanzania kwa sasa wanakopesheka?
Watanzania wengi kwa Sasa hawakopesheki kirahisi ukiangalia Credit rating zao au credit worthness yao imekua ndogo sana, Wengi wameshindwa kulipa mikopo yao walionayo kwa Sasa na hata Bank zikiamua kuuza mali za wakopaji haziuziki kabisa, Je kwa hali hii hizo Bank zikichukua pesa BOT zitamkopesha nani mwenye cash flow nzuri?
Pili, Je kwa kipindi borrowing rate ilipokuwa 9 percent kabla ya sasa, mbona mlikuwa mnalalamika na kuzihitaji Bank za biashara zijitahidi kupunguza mikopo mfu "yaani Non performing loan " Bank zimejitahidi kusafisha vitabu kwa kufuta hii mikopo kwa kuihesabu kama hasara katika mahesabu yao, Ni Bank gani itakubali kukopesha kwa watu wasioaminika?
Tatu :Hii monetary expansionary policy( yaani kuongeza ujazo wa pesa kwenye uchumi kupitia mabenki yaweze kukopesha, Ni Bank gani itayokubali kuingia gharama ya kukopa kwenda kuwakopesha watu wasiokuwa na uwezo wa kulipa pande zote mbili wananchi wamekumbwa na low purchasing power na wafanyabiashara wanapata faida kidogo iliyokumbwa na kodi,
Back to the Topic!
Nini madhara ya BOT kushusha hii borrowing rate upande wa mabenki kulingana na barua yao
1.kutazifanya Bank zishushe riba kwenye fixed deposit za Wateja, Fixed deposit ni pesa ambazo Wateja wameamua kuweka bank kwa kipindi maalumu bila kuzitoa wakitegemea kupata riba, kwa kuwa serikali imeamua kushusha riba mpaka kwenye hati fungani yaani Treasury bills, Hakuna Bank itakayokubali kumlipa mteja wa fixed deposit rate au riba kubwa huku zenyewe zikiwekeza Bank kuu BoT zinapata rate ndogo iliyoshuka kwenye Treasury bills
2.Wateja wengi wataamua kuliquidate pesa zao au Kuamua kuzitoa Benki wakiona wanapata faida ndogo hasa hawa wa fixed deposit
Je wakizotoa Bank watazipeleka wapi wakati kwa sasa hakuna biashara itayokupa return zaidi ya hiyo rate za Bank? Na hata Bank wakikaa nazo hizo pesa watamkopesha nani?
Mwisho,
Naunga mkono serikali kwa hii hatua ya kutaka kustimulate economic growth au kuufanya uchumi ukue lakini hii hatua ya kushusha rate ni nzuri ila kwa mazingira ya sasa watu uwezo na sifa za kukopa zimeshuka, itakuwaje?
Nina uhakika BoT hata kwenye Bank za biashara Kuna watu wanauelewa mpana na wamehudhuria mafunzo toka Basel commitee
Moja ya Sababu kubwa za Benki kushindwa kufanya kazi mmehubiriwa sana na Basel commitee kuwa ni mitaji midogo yaani Minimum capital of Banks below standard, Hapa mmejitahidi kuzifunga Bank nyingi sana za biashara kuwa mtaji hauwezi kuhimili viashiria tata katika uwekezaji yaani Capital /risk weighted assets
Marekani kipindi cha hali mbaya miaka ya 2007 mpaka 2008 alifanya nini?
Moja, Marekani aliamua kuongeza mitaji na pesa kwenye makampuni Makubwa mfano GM au General Motors ili yaendelee kufanya kazi na mpaka sasa GM Motors imesimama na inamalizia kulipa pesa kwa serikali taratibu, kuna makampuni yaliyowezeshwa na serikali Marekani yameshamaliza kulipa madeni kufikia mwaka jana
Marekani aliona bila kuongeza pesa au kuziwesha Bank na kampuni zake angesababisha tatizo kubwa la ajira sana kwa wananchi wake.
Janga kubwa Huo mwaka 2006 to 2008 Marekani aliamua liwalo na liwe Benki kubwa zaidi Marekani Lehman Brothers aliamua bora ife, serikali iliamua kutoisaidia hii Bank kabisa
Kwanini Marekani ilisaidia makampuni na Benki zingine lakini sio Benki kubwa Lehman Brothers?
Nitaelezea kuhusu hii Bank kwenye concept ya "Too big to Fail "Bank kujiona kubwa itasaidiwa hata kama haichukui hatua kuzuia vihatarishi