Maoni kuhusu Katiba mpya ya Jakaya Kikwete, kwanini hayajawa ya uwazi kama ya Jaji Othman Chande?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Jakaya Kikwete alikuwa kiongozi wa waangalizi, kwa upande huu wa Afrika Mashariki, Katika uchaguzi mkuu, uliomazika hivi Katibuni nchini Kenya.

Tulimsikia pia Rais huyo mstaafu, akiwasihi viongozi wawili wakuu, waliochuana vikali Katika uchaguzi huo, William Ruto na Raila Odinga, waliokabana Koo hadi mwisho wa uchaguzi huo, kuwa ambaye hataridhika na matokeo yatakayotolewa na Tume ya uchaguzi wa nchi hiyo aende Mahakamani, kuyapinga matokeo hayo, badala ya kuwahamasidha wafuasi wao walete vurugu.

Tukishuhudia pia uchaguzi huo wa Kenya, ukimalizika kwa amani, bila umwagaji wa damu yoyote

Kilichonishangaza ni kuwa wakati huyo Jakaya Kikwete akiwaeleza hayo viongozi hao wa Kenya, kwenye nchi yake ya Tanzania, kwenye Katiba ya nchi hii, inatamka kwenye ibara ya 41(7) inazuia matokeo ya u-Rais kupingwa Mahakamani!

Tumemshuhudia Rais mstaafu huyo, mara tu baada ya kurudi toka kwenye uchaguzi huo, akiyapeleka maoni yake kwenye kikosi Kazi kikichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya.

Hali ilikuwa tofauti, kwa Jaji Mkuu mstaafu, Othman Chande, ambaye naye alikuwa mwangalizi wa uchaguzi huo, ambaye yeye alijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kueleza tathmini yake kuhusu uchaguzi huo uliomalizika wa Kenya na kuusifu Sana kwa uwazi na kuelezea kuwa Katiba ya nchi yao ya Kenya ni nzuri kwa kuruhusu mgombea ambaye hajaridhika na matokeo, kama yalivyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, kuruhusu kwenda Mahakamani, kuyapinga matokeo hayo.

Sasa ninamuuliza Jakaya Kikwete, akiwa Rais mstaafu wa nchi hii, ni kwanini kwenye Katiba ya nchi yake, hawaruhusu wagombea wa u-Rais kwenda Mahakamani, kuyapinga matokeo hayo?

Hivi Jakaya Kikwete, atayskataaje madai ya muda mrefu ya wapinzani wa nchi hii kuwa Tume ya uchaguzi hii huwa wanafanya "kiini macho" Katika uchaguzi mkuu, huku wakiwa wameshamtayarisha mgombea wa CCM kuwa mshindi wa u- Rais aliyeshinda na ndiyo sababu ya kuzuia matokeo hayo yasipingwe Mahakamani?

Kuepuka nchi hii isije kuingia kwenye machafuko ya umwagaji damu, siku za usoni, ni vyema watawala wetu wa CCM, wakafanya uamuzi wa busara na kuruhusu Rasimu ya Jaji Warioba, ambayo ndiyo maoni ya wananchi wa nchi hii, ikarudi mezani na kuifanya kuwa ndiyo Katiba ya nchi.

Ni vyema Hawa watawala wetu wa CCM, wakayatafakari kwa makini Sana maoni yaliyotolewa na Jaji mstaafu, Othman Chande, kuwa watanzania tusihofu, kuiandika Katiba ya nchi, kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee, ya kuiepusha nchi yetu na machafuko yanayoweza kutokea, iwapo tutaendelea kuing'ang'ania Katiba ya hivi sasa, ambayo ni ya mfumo wa chama kimoja.
 
Back
Top Bottom