MAONI: Kinacho endelea Syria ni vita baridi kati ya Marekani n Russia, kupambana na ugaidi ni changa la macho.

Cybergates

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
652
1,363
Hellow bosess!
Hichi kinachotokea kule syria uangalia kwa umakini unaona hii sio vita ya kupigana na ISIS au sijui ugaidi gani yani paka sasa watu
465000- wamesha fariki
1m- majeruh
12m- hawana makazi (karibu nusu ya taifa zima)
Tokea alipoingia bashar al-assad madarakani syria nayo ndipo ilianza kupata wakati mgumu zaidi kuliko kipindi cha nyuma tukienda kwa haya mataifa mawili (Marekani n russia) ndo nyenye mchango mkubwa huko syria
MAREKANI
Hawa hawajulikani wanataka nini huko syria mpaka sasa hawajawa specific nini wanataka japokua wametumia gia ya kupigana na IS hapo syria na iran, hii kete ndo inawapa kibali cha kuendeleza vita, pia tena hawa jamaa wanampinga Assad wanataka aachie nchi ukifikiria tu IS wanataka Assad atoke marekani nao hawamtaki Assad, hapa unabaki na swali Je **rekani wanafadhili IS?? Pia kuna kipindi trump alisema "Very little to do with syria other than killing IS" alipokuwa anaojiwa na mwandishi wa habar (hapa nimejikuta nawaza viwanda ya silaha na masoko yake)
RUSSIA
ukija kwa hawa watu wenyewe wanaeleweka eleweka sio kama US pia hawa walienda syria kwa gia ya kupigana na makundi yote ya kigaidi yanayopiga serikali ya Assad, hii inamaana kama kuna mtu au kikundi cha watu wanapinga utawala wa assad wata kutana na mrusi. Kama IS ni kikundi cha kigaidi na US hawamtaki assad basi wote wapo kinyume na russia, hii ndo sababu marekani na russia hawapan kwenye vita ya syria..
MAONI YANGU
kama kweli dunia/UN inataka amani iwepo syria lazima Marekani na Russia wakae wafanye mazungumzo bila hivyo vita itazidi kuendelea tu. Mm naona mpambono huko syria ni majingambo ya marekani na russia kwenye kuonyesha nani ame develop advanced military weapon.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom