MAONI KATIBA MPYA:Wabunge kuchapwa viboko na kumwagiwa maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAONI KATIBA MPYA:Wabunge kuchapwa viboko na kumwagiwa maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rwamashugi, Jul 15, 2012.

 1. rwamashugi

  rwamashugi Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wananchi wa wilaya ya Muheza Tanga wameiomba Tume ya Warioba kuwa,Wabunge WANAOSINZIA BUNGENI wapewe adhabu zifuatazo:- Kuchapwa viboko 3
  - Kumwagiwa maji ya baridi
  - Kufukuzwa Bungeni muda wa siku 3
  Hiyo hoja mimi ninaiunga mkono asilimia 100.

  Je wana janvi mna maoni gani?

  SOURCE:Gazeti Mwananchi Tarehe 15 july 2012: Page 7.
   
 2. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Itapendeza sana kwa wabunge wa aina ya RAGE wa SIMBA, LUSINDE na MWIGULU.....
   
 3. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ndiyo hiyoooo
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  Wabunge wanaosinzia wamwagiwe maji, watandikwe viboko – Katiba: Maoni ya Wananchi

  Wakazi wa Kata ya Misalai Tarafa ya Amani Wilayani Muheza, Tanga wamependekeza kuwepo kwa kipengele cha adhabu ya kumwagiwa maji ya baridi na kisha kuchapwa viboko kwa mbunge atakayesinzia akiwa kwenye kikao bungeni.
  Wamependekeza pia kwamba adhabu hiyo iambatane na kutoruhusiwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo pamoja na kuzuiwa kugombea tena kipindi kingine mara muda wake utakapomalizika.
  Walitoa mapendekezo hayo kwa wajumbe wa Tume ya maoni ya marekebisho ya Katiba ilipofika Kijiji cha Misalai kukusanya maoni ya wananchi wa Tarafa ya Amani Wilayani Muheza.
  Shukrani Said (23) ambaye ni mkulima wa Kijiji cha Ziarai Kata ya Misarai alisema kutokana na baadhi ya wabunge kuonekana mara kwa mara kupitia runinga inayoonyesha vikao vya Bunge kuonekana wakiwa wamesinzia kuna kila haja ya Katiba mpya kuwekwa vifungu vitakavyowabana wasilale bungeni, "Wabunge hatukuwatuma waende wakalale, matokeo yake zinapitishwa sheria zinazotubana, tuliwachagua waende wakatuwakilishe, kwa hiyo kuwe na kipengele cha adahabu ya viboko," alisema Shukrani na kusisitiza kuwa adhabu hiyo inavyofanyika ionyeshwe kwenye runinga.
  Richard Lutangilo wa Kijiji cha Bulwa Wilayani hapa alisema pamoja na adhabu ya viboko, Katiba iongeze kipengele cha kumwagiwa maji kila mbunge atakayesinzia na kama haitoshi asipewe ruhusa ya kuhudhuria vikao vitatu mfululizo na pia asiruhusiwe kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo mara kipindi chake cha miaka mitano kinapomalizika, "Hili la viboko likiwekwa kwenye Katiba litaleta umakini wa wabunge wetu kwani tunawaona inatuhuzunisha sana sisi wapiga kura tunapowaona wakiwa wamelala fofofo bungeni wakati vikao vikiendelea," alisema Jacob Zephania.
  Hadi Mlowe (50) mkazi wa Kijiji cha Mgambo alipendekeza umri wa wagombea wa nafasi ya ubunge uanzie miaka 45 kwa kuwa amebaini wabunge vijana ndiyo chanzo cha kukosekana kwa nidhamu ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, "Napendekeza katiba mpya iweke ukomo wa umri wa kuanzia kwa nafasi ya ubunge ili kuondokana na chombo hiki muhimu kukosekana kwa nidhamu tunasikia jinsi wabunge vijana wanavyoropoka linaonekana kama ni Bunge
  la kihuni," alisema Mlowe.
  Cleopas Mutabuzi (50) mkulima wa Kijiji cha Misalai alipendekeza madaraka ya Rais yapunguzwe hasa katika kuteua Mawaziri, ambapo alitaka waajiriwe na Tume ya Utumishi kwa kufuata taaluma zao na siyo kuchaguliwa kisiasa, kadhalika nafasi ya Spika, Naibu Spika na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipendekeza zisitokane na wabunge bali waajiriwe kupitia Tume ya Utumishi na baadaye majina yao yapitishwe bungeni kwa ajili ya kupewa baraka na wabunge.
  Kamati hiyo ya kupokea maoni ya marekebisho ya Katiba ilikuwa wilayani Muheza kwa muda wa siku tatu ambapo iliendesha mikutano huko Majengo, Kwafungo, Mkuzi, Misozwe, Amani na Misalai
  @ mwananchi
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  15/07/2012
  Wakazi wa Kata ya Misalai Tarafa ya Amani Wilayani Muheza, Tanga wamependekeza kuwepo kwa kipengele cha adhabu ya kumwagiwa maji ya baridi na kisha kuchapwa viboko kwa mbunge atakayesinzia akiwa kwenye kikao bungeni.

  Wamependekeza pia kwamba adhabu hiyo iambatane na kutoruhusiwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo pamoja na kuzuiwa kugombea tena kipindi kingine mara muda wake utakapomalizika.

  Walitoa mapendekezo hayo kwa wajumbe wa Tume ya maoni ya marekebisho ya Katiba ilipofika Kijiji cha Misalai kukusanya maoni ya wananchi wa Tarafa ya Amani Wilayani Muheza.

  Shukrani Said (23) ambaye ni mkulima wa Kijiji cha Ziarai Kata ya Misarai alisema kutokana na baadhi ya wabunge kuonekana mara kwa mara kupitia runinga inayoonyesha vikao vya Bunge kuonekana wakiwa wamesinzia kuna kila haja ya Katiba mpya kuwekwa vifungu vitakavyowabana wasilale bungeni, “Wabunge hatukuwatuma waende wakalale, matokeo yake zinapitishwa sheria zinazotubana, tuliwachagua waende wakatuwakilishe, kwa hiyo kuwe na kipengele cha adahabu ya viboko,” alisema Shukrani na kusisitiza kuwa adhabu hiyo inavyofanyika ionyeshwe kwenye runinga.

  Richard Lutangilo wa Kijiji cha Bulwa Wilayani hapa alisema pamoja na adhabu ya viboko, Katiba iongeze kipengele cha kumwagiwa maji kila mbunge atakayesinzia na kama haitoshi asipewe ruhusa ya kuhudhuria vikao vitatu mfululizo na pia asiruhusiwe kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo mara kipindi chake cha miaka mitano kinapomalizika, “Hili la viboko likiwekwa kwenye Katiba litaleta umakini wa wabunge wetu kwani tunawaona inatuhuzunisha sana sisi wapiga kura tunapowaona wakiwa wamelala fofofo bungeni wakati vikao vikiendelea,” alisema Jacob Zephania.

  Hadi Mlowe (50) mkazi wa Kijiji cha Mgambo alipendekeza umri wa wagombea wa nafasi ya ubunge uanzie miaka 45 kwa kuwa amebaini wabunge vijana ndiyo chanzo cha kukosekana kwa nidhamu ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “Napendekeza katiba mpya iweke ukomo wa umri wa kuanzia kwa nafasi ya ubunge ili kuondokana na chombo hiki muhimu kukosekana kwa nidhamu tunasikia jinsi wabunge vijana wanavyoropoka linaonekana kama ni Bunge
  la kihuni,” alisema Mlowe.

  Cleopas Mutabuzi (50) mkulima wa Kijiji cha Misalai alipendekeza madaraka ya Rais yapunguzwe hasa katika kuteua Mawaziri, ambapo alitaka waajiriwe na Tume ya Utumishi kwa kufuata taaluma zao na siyo kuchaguliwa kisiasa, kadhalika nafasi ya Spika, Naibu Spika na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipendekeza zisitokane na wabunge bali waajiriwe kupitia Tume ya Utumishi na baadaye majina yao yapitishwe bungeni kwa ajili ya kupewa baraka na wabunge.

  Kamati hiyo ya kupokea maoni ya marekebisho ya Katiba ilikuwa wilayani Muheza kwa muda wa siku tatu ambapo iliendesha mikutano huko Majengo, Kwafungo, Mkuzi, Misozwe, Amani na Misalai.

  ---
  Burhani Yakub, Muheza.
  Gazeti la Mwananchi
   
Loading...