Maoni juu ya adhabu mashuleni viboko au kusimamishwa masomo na uingiliaji wa wanasiasa kwenye taasisi

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
WAJUMBE SALAAM!

Hivi karibuni kumejitokeza matukio ya utovu wa nidhamu mashuleni na adhabu mashuleni.

Nianze na utovu. Miaka ya leo wanafunzi wameshuka kinidhamu sana. Yapo matukio ya walimu kupigwa, kutukanwa, kukejeliwa na mwalimu anapochukua hatua stahiki wanafunzi huja juu kwa kumtishia mwalimu au kumsingizia makosa makubwa kama kujihusisha na mapenzi na wanafunzi. Mwalimu nguvu humuisha na kuacha kufuatilia wanafunzi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli anasema wamekutwa na simu shuleni wamenyang'anywa wamechoma shule. Tufikiri kwa kina Hivi hill ndiyo sababu au kuna zingine kama hakuna basi huu ni ubabe wa wanafunzi dhidi ya Serikali au walimu wao.

Kuna mtu alinipa stories za huko Mbeya. Kuna shule fulani watoto walijihusisha kimapenzi na wanafunzi wenzao shule ni ya kutwa baada ya walimu kufuatilia wakabaini sio wale wa wawili tu bali kuna pair kadhaa.

Kamati ya nidhamu ikakaa na kupendekeza adhabu iwe kusimamishwa masomo kwa siku saba 7. Diwani wa Kata hiyo aliwarudisha kesho yake shuleni na kusema kuwa watoto wameonewa, mpaka naandika hapa mkuu wa shule hiyo alihamishwa shule na nidhamu ya watoto ndio imeharibika na walimu wanaogopa.

Kama mkurugenzi anavyomuogopa diwani
Diwani darasa la saba mfumo wa elimu na utoaji wa taaluma hajui lakin msomi kama mkurugenzi anasikiliza hata pumba.

Sasa mkuu wa mkoa aliwacharaza kuonesha kutokubaliana nao watoto
huku Diwani anawarudisha wanafunzi shule japo wamesimamishwa kwa vikao halali yupi ana makosa?

Nini kifanyike basi ili wanafunzi WAWE na nidhamu je adhabu zote zitolewe viboko hapana na kusimamishwa masomo tena siku saba nayo isiwepo?

Sisi waafrika bila reinforcement uwe negative AU positive hatuendi
TOA Naomi yako nini kifanyike ili nidhamu iwepo mashuleni? Rejea mifano miwili hapo juu

Ahsante
Naomba kuwasilisha.
 
Suluhisho pekee ni kuzingatia Sheria, Kanuni NA Taratibu mbalimbali za nchi tulizojiwekea.

Wananchi wenyewe washirikishwe kikamilifu ktk kuzitunga hizo Sheria NA Kanuni za nchi.
Mamlaka ya Kutunga Sheria isiachwe KWA watawala peke yao kana kwamba wanatunga Sheria zitakazotumika kuongoza familia zao peke yao,

Sheria zitungwe NA wananchi wenyewe, pia wananchi washirikishwe kikamilifu kwenye hatua zote za utungaji WA hizo Sheria.

Wazazi NA walezi nao watimize wajibu wao wa malezi bora KWA watoto wao ili kujenga jamii yenye Maadili KWA sababu baadhi ya watoto wenye tabia mbaya imetokana NA malezi mabaya waliyopata kutoka KWA wazazi wao ambao nao pia hawana Maadili bora.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, NA maji hufuata mkondo!!
 
Back
Top Bottom