MAONI HURU: Warizi wa mambo ya ndani na IGP wawajibike kwa matukio yanayoendelea nchini!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Inasikitisha sana kuona matukio ya kutisha yanaendelea kuliandama taifa letu huku viongozi waandamizi wanaotakiwa kuhakikisha kua matukio haya yanakomeshwa yapo, viongozi hawa wameshindwa kabisa kua wabunifu kilinda Mali za raia na usalama wao.

Ni miezi michache tu iliyopita waliuawa polisi wetu na majambazi huko Mbande yaliyoambatana na mauaji ya kanda wa vikosi maalum vya kupambana na vikundi vya ujambazi , usiku wa kuamkia leo tena wameuawa askari nane na majambazi, ni kipindi ambacho taifa zima na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania wanapiga kelele juu ya matukio ya mauaji,tukekaji,utesaji na uvamizi yanayofanywa vikundi vya kihalifu, badala yake viongozi hawa wapo wanaendelea kupokea mishahara itokanayo na kodi za Wanyonge hawa.

IGP, uko wapi ubunifu makini wa kua na intellijensia makini ya kuvibaini vikundi hivi vya kihalifu? Kwanini msiwe creative juu ya mambo muhimu yahusuyo taifa letu juu ya usalama wa raia? Intelijensia zenu ni juu ya mikutano ya wanasiasa tu na kukamata wasanii tu au tuwaeleweje? Hivi adui akituingia tutakua tutakua salama kweli? Hofu imetanda hatuna imani kabisa na utendaji wenu.

Katika wilaya Mkuranga,Rufiji na Kibiti kwa ujumla kumekua kukiripotiwa matukio ya kutisha ya kihalifu mara kwa mara jambo ambalo sio geni masikioni kwa watu wengi, mmeshindwa nini kuchukua tahadhari mapema juu ya haya mpaka madhara yajitokeze? Askari wanaopoteza maisha ni hasara kubwa sana kwa taifa maana mafunzo ya kuwatengeneza huchukua muda mwingi na pesa na pesa nyingi, ni watu wenye familia zinazowategemea.

Rais wetu naona amekua mvumilivu sana juu ya viongozi hawa na huenda bado hajauona udhaifu wao juu ya matukio haya, I wish I could be a "President" hakika ningewawajibisha viongozi hawa! Haiwezekani vitendo vya namna hii kuendelea ikiwa kuna viongozi wasimamizi ndani ya wizara na idara mbali mbali za vyombo vya usalama.

Hili suala lingetokea kwenye nchi ambazo viongozi wanazoelewa nini maana ya uwajibukaji sidhani kama mpaka sasa Waziri wa mambo ya ndani na IGP wangekua wanaendelea na nyadhifa zao, ukiona una kiongozi flani na matukio flani flani yanaendelea bila kukoma ujuue kuna udhaifu mkubwa kwenye utendaji wake hivyo huna budi kufanya marekebisho ya uongzi.

Hata TISS nako kuna tatizo pia, maana wao ndio wanaotakiwa kunasa taarifa sahihi juu ya wahalifu hawa ili washughulikiwe kikamilifu,hiki ni chombo muhimu sana kupata taarifa za siri hasa kunapotokea au kuhisiwa matatizo kama haya, na ndio maana nao wanalaumiwa kwa matukio ya ajabu ajabu hasa juu ya utekaji na utesaji unaodaiwa kuendelea dhidi ya raia,inamaana kama wanalalamikiwa kujihusisha na mambo haya inamaanisha kua hawana kazi muhimu zaidi za kufanya kama kupata za taarifa za siri juu ya hawa majambazi wauaji wa polisi wetu.
 
Wanachotaka nyumbu kamwe hakiwi
 
Waziri wa Mambo ya ndani angekuwa tayari ameajibika zamani lakini si katika serikali hii. Kwa nchi yenye kujua hasa majukumu ya usalama wa taifa na kwa mauaji mbali mbali yaliyotokea Rufiji, Mkuranga, Kibiti na eneo hilo, ungekuta wamemwagwa huko wengi. Wengine wanachoma mikaa, wengine wanatafuta kununua korosho, wengine wanatafuta kununua mbao katika mapori hayo, mradi tu wangekuwa wengi huko. Du! Hawa wa kwetu wanasikiliza nyimbo za wasanii huku bongo na kuwakamata na kuwatesa. Vyombo vya usalama humu vimewekeza sana kukabili ukawa badala ya kulinda raia na mali zao. Jumla ya yote,"Twafaa!"
 
Back
Top Bottom