Uchaguzi 2020 Maoni huru: Awamu hii Urais wakipata hata kura Milioni 3 wana bahati sana

Utafiti wako huu kuwa Watu wameichoka CCM uliufanya wapi na lini Mkuu? Na je, hao hao Watu wako wamekuhakikishia wanawapenda Upinzani?
Kwamba Serikali kupata zaidi ya kura 3m itakuwa bahati ni ubashiri wa ndoto za mchana.

Siasa Tz zimebadilika kutoka "mkono mtupu haulambwi" kwani mwenye macho haambiwi tazama.

Wapinzani hawawezi kuungana kwa maana ya kuachiana nafasi za kugombea ngazi zote, pamoja naya Rais, kwa kuwa hilo haliwezekani kwa sababu kuu mbili:
1) Uchu wa madaraka wa wanasiasa waitwe waheshinmiwa na kupata nguvu ya kisiasa kufanikisha malengo yao binafsi.
2) Nia ya viongozi wakuu wa hivyo vyama (vyama vya mifukoni) ili vipate wabunge na wawakilishi ba hatimaye kulipwa ruzuku. Ruzuku ambayo imekuwa ikitumiwa kwa maslahi binafsi ya viongozi wenye vyama badala ya shughuli za vyama.

Wanachoweza wapinzani, ambacho inaonekana hawawezi, ni kuungana katika kushawishi wapiga kura kwa Sera mbadala, hasa za maendeleo, dhidi ya Chama Tawala. CCM kwa miaka mitano inayoisha sasa Serikali yake imefanya mambo makubwa yanayogusa maendeleo ya watu wenye kipato duni (wakulima na wafanya biashara ndogo ndogo) na miundo mbinu yenye kuchochea ukuaji uchumi.

Lakini, lakini, lakini kitakachotokea (kimenza kuonekana) ni wapinzani kuraruana wenyewe baada ya mgombea Urais wa CHADEMA kuwa anekamilisha kejeli dhidi ya Rais na M/kiti wa CCM katika safari zake za kusaka wadhamini. Kampeni zitapoanza, wagombea wa upinzani watageukiana na kushambuliana maana hawataendelea kuisimanga Serikali ya CCM kwa kuwa huo hautakuwa mtaji wa kisiasa kushawishi wapiga kura.
 
Ndivyo ilivyopaswa kuwa lakini tatizo ni wapinzani wa Tanzania .
Tuna wapinzani wa ajabu sana.

Upinzani ndani ya CCM ndio upinzani halisi nje ya CCM ni Vikampi vya watu binafsi.
CCM ya Kikwete ilishindwa na CCM ya iliyokuwa imebeba hasira za Lowasa kukatwa.
Halikadhalika 2025 CCM itakayoshinda ni ile itakayotoka kwa Mtu atakayekuja na hoja za kufanya tofauti na CCM ya Magfl .
Upinzani upo ndani ya CCM.

Leo hii wapinzani kama Chadema wangeruhusu Mageuzi ya ndani na chaguzi huru ndani ya Chama Bila shaka Mwenyekiti angekua ni ama Zito Kabwe au Komu au Heche au Halima. Chama kingekua na mtizamo mpya na nguvu mpya. Leo hii Chadema inaongozwa na MTU aliyeipoteza njia mwaka 2010,2015, 2020 sasa.
Wapiga kura wakimuona Mbowe jukwaani wanapoteza imani ya kushinda. Miaka mitano Mbowe amekua ni MTU wa kulilia Uenyekiti tu huku Chaguzi zikiwa zinavurugwa bila tamko lolote. Sasa kamanda anabaki kwenye kiti na ujasiri wa kujificha nyuma ya shujaa Tundu Lisu.

Kama Kikwete aliwapa watanzania maziwa na nyama na samaki lakini walimkataa kwa kumwita dhaifu asiye na maamuzi na walitamani aondoke madarakani kwa ushawishi wa Mbowe na Dr.Slaa huku wakiamini kuwa nchi inapaswa kuendeshwa kidikteta basi watanzania Chini ya Upinzani wa Mbowe hawawezi kamwe kuiondoa CCM madarakani.

Kwanza Sheria za Uchaguzi zinafanana sana na zile za CCM.
Yani Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wana nguvu kuliko wananchi wote milioni 28+ wanaopiga kura.
CCM wajumbe wa wale wanaopitisha majina Dodoma wapo wachache lakini wana nguvu kubwa kuliko wapiga kura wote ndani na nje ya Chama.

Wapinzani hawana Sera zinazowavutia wananchi zaidi ya kumshambulia Magufuli binafsi. Wakati huo huo wananchi kwa uelewa wao ama mdogo au mkubwa wanazungumza Lugha moja kuhusu Magufuli kuwa ameleta maendeleo makubwa . Yani hata mtu ambaye kijijini kwake hakuna maji ,barabara na dawa hospitalini huku biashara zikiwa zimedoda lakini ana matumaini kuwa Magufuli anabana kwa Muda tu lakini akikamilisha Kujenga miundo Mbinu hali ya maisha itapaa na kuwa nzuri kuliko Ulaya na Uarabuni na tutatoa misaada kwa Wazungu badala ya kuomba misaada. Imani hiyo ipo mpaka kwa wasomi , Wachungaji na mashekhe na wasanii wa Muziki mpaka watoto wadogo ,wazee na wafanyakazi pia wanamatumaini kuwa Hali ni ngumu kwa muda tu. Mpaka kule kusini kwenye wakulima wa Korosho, wote wana matumaini na JPM na wapo tayari kwenda naye kwa matumaini kuwa naye pia ni maskini mwenzao kwa sababu hasafiri kwenda kwa mabeberu kuomba misaada.

Wapinzani wengi hawajui maisha ya vijijini yalivyo kwa uhalisia matokeo yake wanaongelea mambo yasiyo na tija kwa mamilioni ya watanzania huku wakijikita kwenye Hotuba za kumkejeli Magufuli muda wote.
Uchambuzi wako ni sahihi kabisa. Wafuasi wa CHADEMA humu wanasahau kuna kundi la kutosha la wanasiasa wenye nguvu waliokihama chama na ni wagombea wa vyama vya upinzani. Hao wanayajua mambo mengi ya CHADEMA ambayo naamini watayatumia kama mtaji wao wa kisiasa. Hivyo basi, CHADEMA itabomolewa na wagombea wa vyama vya upinzanI na siyo wa CCM.
 
Uchambuzi wako ni sahihi kabisa. Wafuasi wa CHADEMA humu wanasahau kuna kundi la kutosha la wanasiasa wenye nguvu waliokihama chama na ni wagombea wa vyama vya upinzani. Hao wanayajua mambo mengi ya CHADEMA ambayo naamini watayatumia kama mtaji wao wa kisiasa. Hivyo basi, CHADEMA itabomolewa na wagombea wa vyama vya upinzanI na siyo wa CCM.
Hao waliogombea washafeli tayari, leta wengine. Maana hao hata huko waliishia kura 2.
 
Nakitazama hali ilivyo ngumu mtaani, uchumi umekua mgumu kuna mama wanashinda barabarani na nyanya zao na mchicha kutwa nzima hawauzi wanarudisha nyumbani jioni, frame kibao za biashara zimefungwa maeneo mengi, Wafanya kazi wa umma wanalia maslahi duni, mikopo elimu ya juu kizungumkuti mitupu kuna vijana wanalia hawana ada.

Lawama zote ni kwa serikali ya CCM ambayo iliahidi maisha bora kwa watanzania wote na matokeo yake watu wamejikuta katika hali ngumu ya maisha. Wananchi hawa wapo tayari kwa mabadiliko ya kiutawala, sasa kumbe shida siyo Magufuli ni CCM yake.

Aliyofanya JPM tunamshukuru sana anaweza kupumzika akamwachia mwingine kijiti aendelee. Aliyofanya ni makubwa sana na ni fahari kwa nchi historia yake itakumbukwa. Ni mwanzo mzuri kwa mrithi wake.

Wapinzani wakiungana wote wenye nguvu CCM ipo pekee yake hata kura milion 3 hakiwezi kupata. Watu wamechoka wanataka kuona changes za kweli zenye kuleta neema kwa nchi yetu. Wakiungana wapinzani na wanajiandaa bila uoga kusimamia ushindi wao wa haki basi CCM chalii. Tuliona KANU ya Kenya ilivyodondoshwa collaboration ya vyama vya siasa chini ya Mwai Kibaki
Ndugu yangu ogopa sana itikafi na mapenzi ya kisiasa..
Mimi naangalia Zimbabwe, pamoja na dhiki mateso na adha wanayopitia Wazimbabwe bado wapo mashabiki die hard wa ZANU PF. Tena uzoefu unaonyesha kwamba KILA upinzani unavokuwa ndivo ushabiki upande wa pili unaongezeka.
Kikubwa ktk siasa ni matumaini..
Kitu kibaya na tishio kubwa zaidi kwa Upinzani wa Tanzania ni ''Term Limit''...
Wakijua baada ya miaka 10 huyu jamaa ataondoka basi hata Kama amewatenda, watalinda udhibiti wa Dola aondoke aje mwingine.
Aidha ni ukweli ulio wazi wazi kwamba leo HII wanaccm ni wengi zaidi kuliko UPINZANI.
Dhiki na mateso wanayopitia Wananchi sio kipimo pekee
Viongozi wengi Dunia waliowaingiza watu wao kwenye dhiki bado walipendwa na kuheshimiwa sana kwa kuwa waliweza kuwapa watu wao tumaini, kuwapa hadhi, heshima na utu wao kuthaminiwa
 
Ndugu yangu ogopa sana itikafi na mapenzi ya kisiasa..
...
Kikubwa ktk siasa ni matumaini..
...
Aidha ni ukweli ulio wazi wazi kwamba leo HII wanaccm ni wengi zaidi kuliko UPINZANI.
...
Dhiki na mateso wanayopitia Wananchi sio kipimo pekee

Hoja zako tatu hizo zinafikirisha, hasa kwa mleta mada tunayojadili (Rais Magufuli hata kura milioni 3 hafikishi).

Hakuna shaka CCM imejipanga kutumia idadi ya wanachama wake kufanya vizuri kwenye Uchaguzi Mkuu ngazi zote. Wingi wa wanachama na nguvu za Jumuia zake ni mtaji tosha wa kisiasa pasipo kuhitaji nguvu nyingine.

Mapenzi kwa Rais Magufuli kwa jinsi alivyoshughulikia kero za wananchi, hasa jeshi kubwa la wafanya biashara ndogo, wachimbaji wadogo wa madini, wakulima, kina mama kwa huduma za afya, wazazi wenye watoto wa umri wa shule, nk, pia ni mtaji tosha wa kufanya vizuri kwenye Uchaguzi Mkuu.

Hakuna shaka kuwa wananchi wanaona maendeleo ya vitu na kumkubali Rais kwa jinsi anavyotumia vizuri kodi yako kuwaondolea kero za maendeleo yao (miundo mbinu ya usafiri, maji, nishati, afya, elimu, nk).

Ikumbuke kwamba upinzani, katika kipindi chote cha utawala wa Magufuli, wamehangaika, na bado wanahangaishwa na kauli zake, umewaondoa katika kujijenga kisiasa wakiamini kumkejeli, kumdhihaki na kumlaumu, kwao ni mtaji mkubwa wa kisiasa.

Katika hali hiyo, je, upinzani una agenda gani ya kuiondoa CCM madarakani, sembuse wagombea wao kumshinda Magufuli! Mmoja wao tayari amekwisha kujifuta kwenye kinyang'anyiro kwa hoja na lugha anayoitumia kuzunguka nchini, ati kutafuta udhamini. Nyomi ya wanaofika kumsikiliza kwake ndiyo mtaji wa ushindi!!!
 
Back
Top Bottom