Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Je tumchagize na kushinikiza Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili John P. Magufuli? kwa sababu mpaka sasa, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana uwezo wa kumkabili Magufuli kwa vile uwezo wake ni zaidi ya Magufuli?

Kama kawaida yangu, kwenye kila mijadala yenye kuhusisha maoni ya kisiasa, mimi hupenda kuanza kwa declaration of interest kuwa mimi, japo ni mwana CCM, lakini kwenye kutanguliza mbele Maslahi ya taifa ni kama sina chama, sina kambi na sina upande, kwangu ni maslahi ya taifa mbele.

Baada ya rais Magufuli kuingia madarakani na kuanza na zile amsha amsha za uwajibikaji kwa ziara za kushtukiza , zilizofuatiwa na tumbua tumbua, nikauliza humu kama kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli, je tuna haja ya kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?,
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020

Hivyo nikashauri, kufuatia Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuonyesha uwezo wa kuibadili Tanzania, overnight, toka nchi masikini ya kutupa uliyodharaurika, hadi nchi tajiri inayoheshimika, Magufuli aachwe tuu hadi 2025 na hata ikibidi, hiyo 2025 tunaweza tubadili katiba yetu ili rais Magufuli aendelee tuu kama Nkuruzinza, Kagame, Museveni hadi awe kama Mugabe?.

Pia kufuatia trend ya chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema kutoonyesha any seriousness yoyote kuelekea 2020,
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible
nikaconclude kuwa Uchaguzi wa 2020 kwa upande wa urais, litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi kwa ushindi wa kishindo cha walkover kwa CCM.
In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Je Kwa

Lakini kwa mwenendo na matamshi ya Tundu Lissu ya hivi karibuni kumhusu Magufuli, kwa maoni yangu, kwa hapa tulipo, ukimuondoa Zitto ambaye he looks a bit compromised, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani aliyeonyesha angalau uwezo wa kuweza kumkabili mgombea wa CCM kwa Uchanguzi Mkuu wa 2020, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Uchaguzi huo wa 2020 na Magufuli ukapata pata angalau kaji joto joto cha uchaguzi, vinginevyo wapinzani wakimsimamisha mgombea mwingine yoyote, mgombea wa CCM, Dr John Pombe Joseph Magufuli, hahitaji kufanya kampeni yoyote, ni ushindi wa kishindo straight forward kwa kwenda mbele kama ameokota embe dodo bivu chini ya mti wa mwambe!.

Kwa jinsi nilivyomsikia Tundu Lissu na namna anavyoongea, then huyu Tundu Lissu ni typical yuko kama Magufuli type tena yeye ni zaidi ya Magufuli!.

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu, kama, Magufuli ameweza kuchaguliwa kihalali na kumshinda Edward Lowassa, kwenye uchaguzi Mkuu huru na wa haki, then you cannot tell about Watanzania huwa wanachagua nini, hivyo Tundu Lissu ambaye ni zaidi ya Magufuli, akisimama na Magufuli, you can never tell what will happen!, Magufuli naweza akaachwa mbali sana! , ila litabaki swali moja tu dogo, with reference ya kilichotokea Zanzibar, hata huku bara, je ikitokea kweli Chadema ikamsimamisha Tundu Lissu na ikatokea Tundu Lissu akishinda, jee atapewa?.

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

=======
Hoja za wadau

Pascal Mayalla,

Tundu LISU kumpima uwezo wake mpime kwanza kama mbunge. Je jimboni kwake kafanya nini la maana Tangible linaloonekana? Nawasifu wachaga wana msemo kuwa mtu akikuambia ana akili akuonyeshe vitu vinavyoonekana kama vile biashara aliyonayo, nyumba ya kuishi aliyonayo na pesa alizonazo na mali mbali mbali vinginevyo ni mjinga tu sababu akili kwa mchaga haipimwi kwa uwezo wa kubwabwaja maneno kama Lisu afanyavyo.

Ni baadhi tu ya makabila mengine yanayoamini kuwa mtu kuwa na akili ni uwezo wa kubwabwaja maneno ndio waunga mkono Lisu. Mimi binafsi Tundu LISU haja-ni -convince kuwa ni legal or political material. Ni bahati mbaya kuwa hata proffesion kama za wasomi wanasheria ambao fani yao si ya makelele wameingiza na kuruhusu makelele kwenye ofisi za TLS.Hii TLS ya sasa ni too noisy.Serikali iunde tu bodi ya wanasheria this noisy TLS should go to hell. Yaani mtu hata ukiwa ofisi za TLS huwezi tulia kimya u kaconcenrate kuandika defence case ya mteja wako kisa mikelele ya LISU ofisini isiyoisha.

Paskali, Mungu ibariki Tanzania.

Swali lako ni suri. Sidhani kama ulitaka majibu ya ndiyo au hapana. Umetaja majina ya watu ila huwezi kutenganisha na vyama vyao.

Kulingana na chunguzi mbalimbali zihusuzo maswala (issues) ambayo ni kero kwa watanzania; nikirudi nyuma hadi 2012 ni :

  1. Afya
  2. Maji
  3. Elimu
  4. Umaskini
  5. Rushwa/utawala bora
  6. Ajira
  7. Mawasiliano (infrastructure)
  8. Misukumo ya kisiasa( Political pressures)
  9. Upungufu wa chakula
  10. Kilimo.
Mambo hayajabadilika sana pamoja ya kwamba tunaona unafuu kwenye elimu, afya na rushwa. Haya ndiyo yanashuhulikiwa na serikali ya awamu ya tano.

Tunayoyana karibuni kutoka kwa Tundu Lisu ni:
  1. Ukabila
  2. Udini
  3. Udikteta.
Hayapo kwenye kero za wananchi. Ila pia kuyumba yumba kwa msimamo wa Tundu Lisu kuhusu maswala muhimu ya nchi. Mwanzoni walisema awamu ya tano inatekeleza sera ya chama chao, agenda ya ufisadi ikaondoka, utetezi wa raslimali za nchi ukaondoka, nia yake ya kuona nchi inaadhibiwa na mataifa ya nje, na nia yake ya kuona nchi inapoteza amani. kwa hiyo mambo haya ni ya kuangalia. Kukosekana kwa msimamo wananchi wanaweza kukosa imani.

Kushuka pia kwa approval rating ya chama ambamo yumo ni shida pia. Sina uhakika kama Raisi wa awamu ya tano atagombea. Hajasema popote mbali na wapambe wake. Hata asipogomea Tundu Lisu bado ana kazi ya kuwaeleza na kueneza sera yake ya ukabila, udini na udikteta, rasilimali za nchi, amani-kutaja vichache tu- ili jamii imuelewe.

Hapa zilinganishi Tundu Lisu na Raisi wa awamu ya tano; bali Tundu Lisu kwa wananchi wakati wa uchaguzi

Pascal Mayalla,

Pascal naunga mkono hoja yako.

Kuhusiana na swali lako kama Tundu Lissu akishinda atapewa ushindi au la, ni wazi kuwa kwa mazingira yaliyopo hatapewa.

Kwanza ni vizuri ieleweke kuwa CCM bado ni chama dola na Tanzania bado iko katika mfumo wa utawala wa udikteta wa chama (dola). Huu uchama dola na udikteta wa chama kimazingira vimesimikwa kikatiba na kisheria. Mapendekezo ya Jaji Nyalali yaliyokuwa na lengo la kuiondolea CCM hii hadhi ili vyama vyote vya siasa viwe na uwanja sawa wa mapambano ya kisiasa nchini yalitupiliwa mbali.

Sifa moja kubwa ya mfumo wa udikteta wa chama dola ni kukosekana kwa demokrasia ndani na nje ya chama. Hii maana yake ni kwamba, kwa mfano, wananchama hawana sauti katika maamuzi makubwa yanayohusu chama kama nani apeperushe bendera ya chama katika uchaguzi wa urais.

Nafasi ya kutoa maamuzi ambayo yangetolewa na wananchama kidemokrasia kuhusiana na nani awe mgombea urais kwa tiketi ya chama huporwa na kutekwa na kikundi kidogo cha vigogo (kinaitwa deep state) ambacho sio rasmi lakini ndicho chenye maamuzi ya mwisho. Na deep state ikiishamua ni nani awe mpeperusha bendera wa chama dola basi biashara imekwisha; huyo ndiye de facto rais wa nchi. Huu ndio utaratibu unaotumika kwenye mifumo ya kiutawala ya Kikomunisti/Kijamaa na ambao CCM imeurithi.

Kiufafanuzi, itakumbuka mwaka juzi wakati wa kinyang'anyiro cha kumpata mgombea urais wa CCM wajumbe wa kamati kuu (CC) ya CCM Sophia Simba na Emmanuel Mchimbi walishangaa na kuhamaki ni vigezo gani vilitumika "kuwakata" watia nia zaidi ya 30 akiwemo mtu wao. Hii maana yake ni kwamba hata CC kwenye hili suala ilikuwa ni rubber stamp tu!

Ni deep state pia ndio imeweka utaratibu unaofuatwa siku zote (ambao pia sio rasmi kikatiba) wa kupokezana urais kati ya waumini wa dini mbili kubwa nchini. Na haitoshi tu rais kuwa muumini ya moja kati ya hizo dini mbili kubwa nchini, pia ni lazima atoke katika kikundi/dhehebu fulani.

Pamoja na haya maelezo, ni muhimu sana kwa upinzani na hasa Cdm kuwa na mgombea urais mwenye nguvu za kisiasa zinazotokana na uthubutu wake, uwezo wa kujenga hoja, ushawishi na weledi. Kama ulivyosema katika kambi ya upinzani mwenye hizi sifa kwa sasa ni Tundu Lissu pekee.

Lakini ni muhimu zaidi kwa upinzani kuweka mikakati makhsusi ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wabunge na madiwani. Lengo kimkakati liwe ni kufikia uwiano wa idadi ya wabunge katika bunge na madiwani katika mabaraza utakaowezesha kuwepo kwa checks and balances; kitu ambacho ni muhimu kwa demokrasia kushamiri pamoja na kuwepo kwa uwajibikaji.

Nitarudi ili kujaribu kutegua hiki kitendawili: "Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!"
 
Umeongea ukweli Mchungu ambao chama Chetu Pendwa sana CCM hakitaki kuusikia.Ukiniuliza nitasema hivi,kama siyo Lissu basi 2020 tunatakiwa tumeweke RAIS ambaye ni purely mwanasheria,siyo mwalimu wa chekechea wala wa secondary tunahitaji mwansheria.

Ukiangalia nchi nyingi duniani zimeendelea kwa kuwa na Rais mwanasheria,tukiangalia Zimbabwe first Lady wa enzi zile alikuwa Mwanasheria na alimsaidia sana Mugabe kuiweka Zimbabwe kwenye mstari,alipokufa Mama yule na Mzee kuchukua chicken & Chips,uchumi wa Zimbabwe ulidondoka kama mvua ya mawe.

Angalia Clinton na Obama wote ni wanasheria ona walivyojenga Uchumi wa Marekani,na leo muone Trump anachofanya kutwa kucha kugombana na wanaomkosoa,hana tofauti na Baba J.

Kama tungekuwa na Tume huru hakika TL fits for presidency.
 
Duh! Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi!

Eti Tundu Lissu ni zaidi ya Rais Magufuli! Kwa wanaojua maana tumeelewa una maanisha ni zaidi kwenye 'kuropoka ropoka'.

Kama CHADEMA wanazo pesa za kumrudishia Lowassa alizowapa ili awe mgombea wa kudumu then Mtu yoyote anaweza kuwa mgombea kwa tiketi ya CHADEMA achilia mbali Tundu Lissu.

Kwa trends zinavyokwenda kuna uwezekano mkubwa hata wabunge wa kambi ya upinzani watapungua baada ya uchaguzi 2020 bila kujali nani atakuwa mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.
 
Duh! Ama kweli alitukanaye hakuchagulii tusi!

Eti Tundu Lissu ni zaidi ya Rais Magufuli! Kwa wanaojua maana tumeelewa una maanisha ni zaidi kwenye 'kuropoka ropoka'.

Kama wanazo pesa za kumrudishia Lowassa then Mtu yoyote anaweza kuwa mgombea kwa tiketi ya CHADEMA achilia mbali Tundu Lissu.

Hakika ni zaidi ya Magufuli, kwanza hana mascandle yule mwenyekiti wenu wa Chama Cha Makinikia si ndiye aliyetuletea kivuko kibovu kwa bilioni nane? Au si ndiye aliyekwapua nyumba za serikali akagawa kwa wadada na nduguze?
 
Hakika ni zaidi ya JPM,kwanza hana mascandle yule mwenyekiti wenu wa Chama Cha Makinikia si ndiye aliyetuletea kivuko kibovu kwa bilioni nane?Au si ndiye aliyekwapua nyumba za serikali akagawa kwa wadada na nduguze?
Hivi kwanini mnajitoa akili? Hizo nyumba za selikali aliuza chini ya boss wake Sumaye, na mnae huko chadema, mfukuzeni huko ili tujue kweli hicho chama chenu hakilei mafisadi
 
Back
Top Bottom