Maoni: Halima Mdee na wenzake wajiuzulu ubunge kuungana na CHADEMA kumpigania Mbowe

Wadau nawasalimu,

Nichukuwa nafasi hii kuwashauri japo sio lazima kuufuata ushauri wangu Wabunge 19 waliofukuzwa Chadema yaani Halima Mdee na wenzake.

Naamini wao binafsi wanaujua ukweli uliowafikisha bungeni ulivyoratibiwa na Magufuli, Tume ya Uchaguzi na bunge na sio chama chao lengo likiwa kukiua chama chao walichokijenga kwa jasho na damu.

Leo kiongozi wao Mh. Mbowe kakamatwa na kabambikiziwa kesi ya ugaidi na hao hao waliowapeleka bungeni

Nawashauri kama kweli mna dhamira ya dhati ndani ya mioyo yenu juu ya Chadema basi ni wakati huu sasa wa kuungana na wanachama wenzenu kumpigania kiongozi wenu mkuu Mh. Mbowe ktk kesi inayomkabili.

Mnachotakuwa kukifanya ni kujiuzulu ubunge wenu naamini wanachama wa Chadema watawapokea kwa vifijo na nderemo na kuwasamehe ili muungane kumpigania kiongozi wenu kwa pamoja na Watanzania pia watawaita mashujaa wa siasa kandamizi za CCM.
Ushauri wako waweza kuwa mzuri na pia waweza kuwa si wabusara, ni kama kusema;
'kwasababu baba wa familia amekamatwa na kusingiziwa kesi, basi wana familia, mama na watoto waache kazi na masomo kuonyesha kumsapot baba' kama baba ana hekima akitoka lazima awapige makofu. Ni mtazamo wangu tu. Naamini zipo njia bora zaidi
 
Esther Matiko, Esther Bulaya, Halima Mdee, yaani hawa madada zamani walikuwa wakiongea watu tunawasikiliza ila sasa sio wapo hai wau vp?!
Hawa ndio cdm ya ukimwaga mboga tunamwaga ugali, acha hawa wako Space ya Maria Sarungi , ni toleo fake
 
Back
Top Bottom