cbandiho
Member
- Sep 2, 2012
- 67
- 47
Bila kupepesa macho,kama bunge letu litaacha hili swala la madini lipite hivihivi,basi bunge letu litakuwa la ajabu kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea.
Kwa mujibu wa katiba yetu ya jamhuri bya muungano wa Tanzania,Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina sehemu mbili,yaani Rais na Wabunge.
Upande wa Rais wetu ameshatekeleza wajibu wake,upande uliobaki ni wa wabunge wetu.
Sasa wabunge wanatakiwa wafanye nini kwa sasa
1.Kujadili mikataba yote ya madini.wabunge kwa pamoja waombe mikataba ya madini ijadiliwe bungeni na hili naiman kwa sasa linawezekana kwa sababu pande zote mbili yaan CCm na Upinzani ztaafikiana katika hili, kama upinzani watapeleka hoja hii basi CCM wataogopa kuonesha unafiki wao kwa sababu watakinzana na Rais
2. Bunge liwahoji mawaziri wote na makatibu wakuu wote wa wizara ya Nishati na madini waliopita tangu mikataba hiyo kusainiwa ili kujua kwa nini waliruhusu huo wizi kwa taifa letu kwa mda wote huo.
3. Bunge liwahoji marais waliopita kuhusiana na mikataba waliosaini ya madini yetu ili wawafafanulie watanzania wanaoamini kuwa mikataba hiyo ndiyo chanzo cha wizi huu tunaoambiwa na unaoendelea kultafuna nchi yetu
4. Bunge liazimie kuwawajibisha wote waliohusika kwa namna yoyote ile kufanikisha uharamia huu wa rasilimali zetu katika nchi yetu,ikiwezekana hata wenye kinga waondolewe ili kujibu tuhuma hizi.
Hizi hoja hata kama CCM watazipuuza , upinzani ni bora mkasimama kidete,hata kama mtatolewa nje au kupuuzwa basi watanzania wataelewa unafiki wa CCM katika swala hili la madini.
Rais wetu katuonesha njia ni bora tukamsaidia kufika hko tulipopigia kelele siku zote,tukimwacha peke yake katika hili tutakaoumia ni sisi watanzania.