Maoni Binafsi Kuhusu Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Disclaimers: Haya ni Maoni BINAFSI. All interests declared. All due respect accorded. Emphasis added. Some mistakes MIGHT have been made while referring to the Bill.

AWALI: Pongezi nyingi kwa wahusika kwa kuleta muswada wenye malengo maridhawa ya kuboresha elimu.

USULI: Binafsi, hupenda fumbuzi zinazotegemea soko-huria (market-based solutions), na ambazo huacha wananchi wakiwa huru kutumia hiari yao kufanya maamuzi. Hii hupunguza ukubwa wa vyombo vya umma, na kuongeza ufanisi na kukuza uchumi.

MAONI: Kwa kifupi, maoni yangu yanalenga kuuboresha muswada ili uendane na misingi ya fumbuzi za soko huria. Pili, umma uuachie sekta-binafsi ijiratibu yenyewe. Hivyo sheria hii ibane tu walimu walio kwenye ajira yautumishi wa umma. Na kisha, Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania, iwe na majukumu ya kishauri na kisera. Isifanye kazi za kukimbizana na mwalimu mmojammoja. Ndio maana ya Bodi. Si ndio?

EDIT: Maoni yenyewe yako kwenye kiambatisho, ambacho kimeboreshwa.

EDIT: Further readings: Dunia inaelekea kwenye shule-huria. Msisitizo ukiwa kwenye HURIA.

A Basic Guide to Open Educational Resources - Wikisource, the free online library

A Basic Guide to Open Educational Resources/Appendix 5 - Wikisource, the free online library

https://www.curriki.org/

TESSA | Teacher Education in Sub-Saharan Africa (TESSA)

OER Africa

Home: The National Institute of Open Schooling (NIOS)

List of Registered Open Schools


Note to mods: kindly leave it here; do not merge with anything.
 

Attachments

  • CommentsTabulated.pdf
    140.6 KB · Views: 17
Mkuu Mlenge nimeyasoma maoni yako, umejitahidi sana kuweka sawa vifungu, big up brother

1. Roving teacher haijafafanuliwa kama ni member of the teaching staff of a school ?
Kama ndivyo kifungu kipo sahihi, kama sivyo recommendations zako zipo sahihi

2. Nakubaliana nawe, professional teacher ni yule anaye adhere to code of ethics
Planner au Quality assurance siyo lazima awe professional teacher

Hili limefafanuliwa vizuri na professional nyingine kama Doctor, Nurse, Pharmacist

Professional hizo zimeweka wazi nani ni DR, Pharmacist au Nurse

Wengine wanaitwa supporting staff hata kama ni sehemu ya medical teams

3. Kuhusu wajumbe wa Board, ni vema wakatajwa wanapaswa kutoka eneo gani

4. Mswada huu ni kwa Walimu wa Tanzania.Zanzibar wana vyuo vyao na taratibu zao za usajili.

Neno Tanzania lingeondolewa iwe Tanganyika, kama ilivyo Tanganyika medical board
Likiachwa kama lilivyo, mtu atatoka Zanzibar na kupata usajili kwa jina la Tanzania wakati std ni tofauti.

Uteuzi wa wajumbe unaweza kuleta mzozo kwa ZNZ kusema haikushirikishwa kwavile ni jina la Tanzania

Uteuzi wa Wazanzibar utaleta tatizo kwasababu ni tofauti na hawatasimamia ipasavyo chombo kisichowahusu

Kwa ufupi, mswada una matundu mengi na ningeshauri wadau waupitie kwa makini

Ahsante kwa angalizo
 
Back
Top Bottom