iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,438
- 14,916
Kuna baadhi ya mambo ukiyaona yanatia haya moyoni, kuna baadhi ya mambo Serikali inajiumbua yenyewe na kujiaibisha, mfano mzuri ni pale Bandarini
haya mambo yalitakiwa yamalizikie ofisini.
Rais amwite waziri anayehusika na bandari, amwite Mkuu wa Bandari pamoja na watendaji wote, amwite Mkuu wa Taasisi ya vipimo kuhusu masuala ya mita, awahoji akiwa na kamati yake inayomshauri kuhusu hayo (kamati hiyo iwe well informed na ihusishe watu wa sekta binafsi na umma kila mmoja imshauri kwa wakati tofauti).
Baada ya kuhojiana nao labda angejua kwa nini flow meter za mafuta hazijafungwa na kwa nini mashine za ukaguzi ziko chache, pili rais aweke maeneo nyeti kiuchumi ambayo yatatakiwa kutoa taarifa kwake kila mwezi au wiki mbili. Nne, rais ashauriwe kuhusu baadhi ya sekta ambazo zinaweza kuupeleka uchumi mbele kwa haraka na mgawanyo mkubwa ki nchi hivyo kuupeleka uchumi mbele, mfano utalii, kisiwa cha Rubondo kina uwezo wa kuwavuta watalii Geita na Burigi na hata Bukoba, cha msingi ni uwekezaji tu.
Kile kisiwa ukifanyika uwekezaji, pamoja na visiwa vyote vya ziwa Viktoria, Nyasa, Tanganyika, Bahari ya Hindi tutapata hela nyingi za kigeni, utalii unalipa sana na baraza la mawaziri limwambie rais hivyo.
Tuna haja ya kupanua mawazo kuhusu kusogeza nchi mbele. Sasa tunahangaika na vitambulisho lukuki vya nchi. Makampuni ya simu yamejitahidi kututoa kwenye mabunda ya noti. Tulitaraji vitambulisho vya taifa vituwezeshe kununua bia baa, tiketi ya ndege kwa kuwa na programu maalum ya kielektroniki inayowezesha kuhifadhi taarifa kadha wa kadha ikiwemo TIN number.