#COVID19 Maoni au ushauri baada ya kuchanjwa Chanjo ya Uviko-19 kama shuhuda! Umepata changamoto ?

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
889
1,515
Binafsi nimepata chanjo ya uviko-19 nchini Tanzania; lakini sijapata mpaka sasa maudhi madogo wala makubwa na hivyo namshukuru Mwenyezi Mungu kuniepusha changamoto walizopata wenzangu wachache nchini Tanzania. Je, nini maoni au ushauri baada ya kuchanjwa Chanjo ya Uviko-19 kama shuhuda ! Umepata changamoto ? Elezea hapa.

1628165805715.png



Wataalamu wa afya wamesema mtu aliyepata chanjo ya corona anaweza kuumwa kichwa, kupata homa, kusikia baridi, kutapika na mwili kuuma saa chache baada ya chanjo au hasipatwe na maudhi hayo baada ya kupata chanjo za uviko-19 (Covid-19) 🇹🇿

Kumekuwa na shuhuda za changamoto kwa baadhi ya watu waliopata chanjo ya Janssen au Johnson&Johnson, iliyoanza kutolewa nchini Julai 28,2021 kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kuizindua rasmi; kwa mujibu wa gazeti la mwananchi ukisoma makala ya Wasemavyo madaktari yanayoweza kutokea.

1628165675717.png


Mwisho niombe watanzania wenzangu tuepuke mawazo potofu dhidi ya chanjo ya uviko-19 yanayosambazwa hasa kwenye mitandao ya jamii na kuleta hofu kwa watanzania waliokosa elimu sahihi ya chanjo za corona na kisha wakaangamia kwa kukosa maarifa sahihi.

Nawakilisha wakuu pamoja na pdf ya majibu ya maswali yanaulizwa na watu wengi kuhusu chanjo za covid-19. Asanteni!
 

Attachments

  • maswali na majibu kuhusu chanzo ya covid-19 pdf.pdf
    224.3 KB · Views: 14
Wakuu naomba niwajulishe kwamba baada SAA 18 nilianza kupata changamoto ya maudhi ya baridi Kali na baadaye joto Kali kwenye mwili wangu usiku wa kuamkia leo !

Ni kama homa sasa imejitokeza na kichwa kinaumu ingawa nimeamka na kuendelea majukumu ya kila siku kwa rehema zake Mungu.
 
Back
Top Bottom