Maoni au Mrejesho wa wateja ni muhimu sana katika biashara

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
4,393
7,037
Sio jambo jingine ni hili la kuweka namba ama kisanduku cha maoni ya wateja kuhusu biashara yako!

Wateja pia wamekuwa wanakumbana sana na dharau za wafanyakazi either Dukani ama sehemu mbalimbali za biashara na kushindwa kabisa wamlalamikie nani!

Na uwamuzi wanauchukua ni kuhama hiyo sehemu kabisa na kupata hiyo huduma sehemu nyingine, kwahiyo hapo anayeumia sana ni mmiliki wa biashara husika!

Nakuambia kuna wafanyakazi wana dharau dunia hii we acha tu, pesa ya kwako bado usujudie! Inakera sana.
 
Back
Top Bottom