Maongezi 'yoliyovuja' ni onyo kwa wanasiasa

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Hivi punde nimesikiliza yanayosemekana ni maongezi kati ya Nape na wanasiasa wawili, Kinana na Ngeleja. Kwa mimi binafsi naamini bila shaka hizo ni sauti zao na hayo maongezi yalifanyika.

Sasa ' kuvuja' huku kumeniacha na maswali yafuatayo ambayo nafikiri nayajua majibu yake.

Ni chombo gani chenye uwezo wa kurekodi maongezi ya watu kwenye simu hapa nchini?

Je haya maongezi 'yalivuja' kama tunavyosikia? Kama la ni nani alitoa ruhusa yasambazwe?

Kama yamesambazwa nini nia ya msambazaji?

Yawezekana msambazaji anawaonya waongeaji kwamba anawasikiliza na anajua wanachokifanya?

Ushauri - (**fanya utafiti kabla hujajaribu) - Muwe mnatumia WhatsApp kwenye maongezi nyeti kwasababu mawasiliano yako encrypted. Ni vigumu kwa mtu anayetaka keyanasa maongezi kujua kinachoongelewa. **Lakini, pia kuweni makini kwasababu najua serkali za Marekani na Uingereza zilikuwa zinawalazimisha watengenezaji wa hiyo App, WhatsApp kuwapa uhuru wa kusikiliza na kusoma maongezi ya watu. Sina shaka serikali za Marekani na Uingereza zinaweza kuyanasa mawasiliano kwa njia ya WhatsApp lakini sina uhakika kwa nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom