Maongezi ya Mke na Mume: Nani yupo sahihi hapa?

Sio kuzaa tu, ana wajibu wake lakini siyo kukulipia kodi ya nyumba na kukusomeshea wanao.
hivi ndo vitu nakataa mimi....mwanamke mwenye akili hawezi kumwachia majukumu mwanaume pekee...eti unafanya kazi kila kitu mimi...tunagawana miezi hii unalipa kodi, miezi ijayi ni mimi,, na vitu kama hivo...

Hakuna kitu napenda kama wote tukiwajibika.
 
Demu akiamua atoe boko hana sababu, ni kama mchawi tu,... Simamia msimamo kama kiongozi na mwanaume wa familia... Acha kujenga hofu ya kuchapiwa, utakua bwege,.... Mke hana dhamana...

Usiuze madarakani yako katika uongozi wa familia...

Sent using Jamii Forums mobile app
daah mkuu umenena cha maana sana.Na huu ndio ukomavu wa kifikra Eti unaogopa kuchapiwa kisa hutoi huduma...Mwanamke hana guarantee unatoa huduma na anachapwa vile vile...
 
Ndo maana wanaume wengi wanakufa mapema sababu ya huu upuuzi unaozungumzia...
Hakuna kitu kizur kama kushirikiana katika kufanya maisha..Mwanaume anakua na stress tu..Aiseeh nikiwa nina mwanamke anapiga kazi tunagawana majukumu hataki anatembea..maaan wanawake wanatofautiana kimtizamo..kuna mwingine yupo kwa ajili ya kufanya maisha anakua sio selfish...
Angalia...kodi mimi, ujenzi mimi, chakula mimi, shule watoto mimi, mikopo+madeni mimi, hela ya mwanamke inafanya nini!!
Katika maisha yangu sitaki kujiumiza na kubeba kila kitu mimi...Life is too short ni kuinjoy na sio kuteseka for the sake of a woman au hiyo unaita majukumu...To me Nop
Umenena vyema, mbona hujaongelea wale mama wa nyumbani wasiokuwa na kazi yoyote ya kumuingizia kipato?

Hao ndiyo nao wazungumzia mm na siyo hao wanawake wa ofisini wanao lipwa milion 3
 
Hii sio sahihi...ndoa ni kusaidiana katika majukumu yote ya familia na sio kumtegemea mmoja atimize majukumu

Wanawake tuna nafasi kubwa kuchangia kipato cha familia na kwa kufanya hivyo hata maendeleao ya familia yanaongezeka na maamuzi ya pamoja yanakua na tija

Ulimwengu huu hakuna kusema mume ndio abebe majukumu yote ya mahitaji ya familka tunapaswa kuwahurumia waume zetu na kusaidiana nao katika kile hali...hii pua ni njia ya nkuongeza upendo na heshima katika familia

Unless kama mtu ni mama wa nyumbani hana kipato vha namna yoyote lakini pia mwanamke hupaswi kubweteka kukaa tu bila kujishughulisha japi hata na kilimo cha mbogamboga

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma tena ulivyoandika "........tunapaswa kuwahurumia waume zetu". Kumbe ukimsaidia jambo mumeo ni kwamba umemhurumia, sio wajibu wako.
Tazama neno lingine uliloandika :".....kusaidia".
Kumbe mke humsaidia tu mumewe, na tafsiri yangu ya kusaidiwa ni pale ninaposhindwa. Haiwezekani unifanyie kitu ninachokiweza halafu useme umenisaidia.
Kwa hiyo ni sawa, mume anaposhindwa asaidiwe lakini vinginevyo atimize wajibu wake.

Tahadhari: MISAADA NI CHANZO CHA MASIMANGO. Na hii huathiri nguvu za kiume.
 
huna mke wewe.. unajua maana ya ndoa? maana ya kuwa mwili mmoja? kama umeelewa hiyo flow matunzo ni ya mume but si kwamba mke akifanya hivyo palipo na uwezekano alipwe.. wao ni familia tayari hakuna changu kuna chetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nina mke na watoto na ninawatunza wote. Katika maisha tuliyoishi nimewahi kukwama mara kadhaa mke wangu akanisaidia na mara zote nilimshukuru kwa unyenyekevu mkubwa kwa kutambua kuwa amenisaidia katika wajibu uliokuwa wa kwangu. Na siku aliposema ananikopesha nilimlipa pesa yake. Kwa mfano, kuna wakati mwanangu alipata changamoto shuleni katikati ya semester nikalazimika kumhamishia shule nyingine, mama yake akanikopesha pesa kutoka kwenye mradi wake wa kuku nikamlipia mtoto shule nyingine, zile pesa nilikuja kumrudishia kama nilivyokuwa nimemwahidi.
Wajibu wa mwanaume uko palepale, mkeo akikusaidia haibadilishi ule wajibu sasa ukawa wa kwake.
 
Hiyo pesa kaipata wapi... Tuanzie hapo kwanza... Unajua nyie akili zenu hizo ndio maana ndoa zinawashinda

Sent using Jamii Forums mobile app
Source ya pesa za mwanamke, ilimradi ni halali, haibadilishi hizo pesa zikawa za kwako. Hata kama umempa, ukishampa ni zake ana uhuru nazo. Kwa mfano leo umempa mkeo sh milioni moja zawadi, halafu kesho una shida ya laki mbili, ukiitaka itoke kwake inakubidi umwombe na ana haki ya kukubali au kukataa kwa kuwa fedha sasa ni za kwake. Pia ana haki ya kukukopesha na una wajibu wa kuzilipa kama utazikopa.
 
hivi ndo vitu nakataa mimi....mwanamke mwenye akili hawezi kumwachia majukumu mwanaume pekee...eti unafanya kazi kila kitu mimi...tunagawana miezi hii unalipa kodi, miezi ijayi ni mimi,, na vitu kama hivo...

Hakuna kitu napenda kama wote tukiwajibika.
Mwingine wa Dar huyu. Uanaume mgumu babake, kama suruali mbona hata wanawake wanavaa?
 
From the Topic huyo mwanamke ni mchoyo, kwa tabia hizo hata mamaako mzazi akija kukutembeleeni itakuwa sio ajabu kushuhudia michicha na marage vikipikwa mfululizo hata kama friji limejaa nyama na samaki!

Hio tabia iko kwa wanawake wengi ila binafsi nilishaipiga marufuku kwa mtarajiwa wangu toka niliposikia ameanza swaga za changu, yangu sijui n.k

Ubinafsi,Choyo na lolote la kushahibiana na hayo nilivipiga vita mapema na sitaki kuviona katika maisha yangu na ikishindikana basi sioni sababu ya kuendeleza mapenzi. Kama baba nitawajibika kwa kadri niwezavyo ila nikikwama bibie ajue kabisa kunipiga tuff sio dhambi kabisa.

I thank God amekuwa muelewa sasa kuwa life lina milima na mabonde, still moulding her though to be the best woman kabla hajavaa pete na kuanza uzazi wetu.
Heh! Kumbe hujaoa? Ok, jifunze taratibu.
Ni sahihi mwanamke kukusaidia, lakini si wajibu wake. Mwanamke anaweza kukusaidia hata mambo makubwa sana, lakini si wajibu wake, ni mapenzi. Na mapenzi si wajibu, ni hisia. Na hisia hutunzwa na kulindwa.
Kwahiyo ukitaka mkeo akufanyie hata yale ambayo ni wajibu wako, na ayafanye kwa furaha bila manung'uniko wala masimango, wewe mpende tu, mwoneshe mapenzi ya dhati, mpe utulivu na amani ya ndani, mpe uhakika na kujiamini. Atafanya mengi sana kwa kadri ya uwezo wake na mtastawi.
 
mimi sio wa dar nipo mkoani...kanda ya ziwa kama wewe ni Ke....nitafute utapata huduma nzuri ukija
Pole, mimi siyo ke. Lakini hao ke kama unavyowaita, kama hujampata wa maisha, basi inabidi wachukue tahadhari sana na mwanaume wa aina yako anayetaka kugawana majukumu yake na mwanamke.
Ni kanda ya ziwa ya wapi hii inayotafuta mashindano ya kugawa majukumu ya kiume yaende kwa wanawake?
 
Pole, mimi siyo ke. Lakini hao ke kama unavyowaita, kama hujampata wa maisha, basi inabidi wachukue tahadhari sana na mwanaume wa aina yako anayetaka kugawana majukumu yake na mwanamke.
Ni kanda ya ziwa ya wapi hii inayotafuta mashindano ya kugawa majukumu ya kiume yaende kwa wanawake?
Acha ku complicate maisha kijana!!
 
MKE: Naomba nilipe hela ninayokudai

MUME: Hela ipi mke wangu unayonidai?

MKE: Wiki iliyopita nilitumia hela yangu kumnunulia Sara madaftari, halafu juzi Rama alikuwa anaumwa nikamnunulia dawa kwa hela yangu, halafu wiki nzima mboga nimenunua kwa hela yangu. Hukuniachia hela yoyote uliposafiri kwenda kazini. Jumla nakudai 2,2500. (Elfu 22 na 500)

MUME: OK, kwani Rama na Sara ni watoto wa nani?

MKE: Ni wangu mimi na wewe.

MUME: Kwahiyo, uliwauzia huduma ulizowapa mpaka nikulipe?

MKE: Hapana, lakini nilitumia hela yangu binafsi, nilipe mimi bwana

MUME: Nitakulipa, ila nikifa naacha wosia watoto wakalelewe kwa mama yangu mzazi.

MKE: Kwanini wakati nipo?.

MUME: Kwa kuwa utatumia hela yako kuwahudumia halafu utaanza kuwadai kwa vile huwahudumii bure bali ni biashara. Halafu mke wangu hivi mimi hela nazotafuta ni za kwangu au ni za mimi na wewe na watoto? Hizo zawadi nilizowaletea wewe na watoto utanilipa kwa kuwa nimetumia hela yangu?

MKE: Lakini hela hiyo nili....

MUME: Wewe ni msaidizi wangu, ubavu wangu. Chako ni chetu, changu ni chetu. Nikikulipa tafsiri yake wewe ni mfanyakazi au hawara na si mke. Au una mume wa kumsaidia kutunza familia zaidi yangu?

MKE: Nipe hela yangu Baba Sara, la sivyo utajuta.

MUME: Na wewe lipa kodi ya nyumba yangu, la sivyo ondoka.
Haya ni ya kawaida sana kama unawajua wanawake I have handled more than 5 similar cases na hii.

Hela ya mkeo ni ya kwake binafsi ila ya kwako ni ya familia.

Ukiwa mwanaume lazima uyajue haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyu mwanamke lengo lake ni nn
Kwan yeye si mama na nijukumu lake kulea watoto
Siku zote mama anatakiwa kuwa lea watoto sawa na baba
Sasa pale mama unataka kulipwa kunatofauti gan na malaya , au mwanamke anayekuzalia watoto lakin hamuiishi pamoja.
Mda mwingine kama mwanamke tumien busra na sio kila kitu ni visasi au kulipana lipana . Kwani wote si mlihusika katika kuleta watoto humu duniani. Basi waleeni kwa pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom