Maonesho ya Wagonjwa na vifaa vya tiba Muhimbili Hospital

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,165
Siyo niya yangu kurudisha mjadala uliowahi kuchemka kwa nguvu hapa JF. Najaribu kuonyesha kumbukumbu tuliyonayo.

Najiuliza jinsi siasa inavyo vuka mipaka yote ya sheria na utu hapa Tz. Ni wiki kadhaa sasa nimekuwa nikiona marudio ya vipindi vya mafanikio ya Hospitali ya Muhimbili. Sehemu kubwa ya maelezo hayo inatokana na ziara ya Rais akiwa na waziri wa afya ktk hospitali hiyo nadhani akifungua jengo ambalo litakuwa na huduma ya upasuaji wa moyo. Nadhani pia ni mafanikio ya kisiasa.

Huko nyuma kuna madaktari wa hapo hapo Muhimbili waliwahi kujitokeza kwa majidai ya kulinda kitu ‘ethics’ pale Dr Masau wa Tanzania heart Institute alipojitokeza kueleza uwezo wa institute yake. Ilionekana kafanya makosa ya kuadhibiwa kwa kuonyesha wagonjwa na vifaa au uwezo wake. Kujitangaza.

Haya ya muhimbili sasa hivi ni nini? Au kama ni hospitali ya serikali hakuna ‘ethics’ inaruhusiwa kujitangaza na kuonesha vifaa na wagonjwa waliolazwa kama ilivyo sasa hivi?

Hao waliojidai kuna ethics za u-daktari wako wapi sasa? Au wanadhani hatuna kumbukumbu ya hayo waliyoyaeleza siku za nyuma. Fallacy!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom