Tetesi: Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ( SABASABA ) kudorora tena kwa mara nyingine

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,419
215,177
Yanaitwa Maonesho ya biashara , lakini ukweli ni kwamba pamoja na bidhaa kadhaa kuonyeshwa , Wafanyabiashara tumetumia nafasi hiyo kuuza , tena kwa mauzo ambayo huvunja rekodi .

Sasa kutokana na kwamba almost 85% ya wateja wetu ni hawa wananchi wa kawaida ambao wamepigika vibaya sana kiasi cha kushindwa hata kumudu milo mitatu , basi tutegemee maumivu.

Sababu za kupigika kwa wananchi wa Tanzania zinafahamika .

Nachukua nafasi hii kuwatahadharisha wafanyabiashara wenzangu kwamba MAONESHO YA MWAKA HUU NI MAONESHO KWELI , NA WALA SI MAUZO TENA KAMA MLIVYOZOEA
 
Kwa kuzingatia uzoefu maonesho ya aina ile na maudhui Yake ni kuwa ilipaswa Watu wawe wanaingia bure ili mradi kunakuwa na umakini mkubwa ktk kuzingatia ulinzi na usalama Kwa ujumla wake ndivyo nchi nyingine kufanya, sasa haya ya hapa kwetu sijui Kwa nini wanataka Watu waingie Kwa kulipia ? Yani kwenda kuona bidhaa au huduma zinazozalishwa au kuuzwa na Watu au makampuni Mimi mwananchi nilipie? yani ni Kwa mfano Mtu anataka kuingia Kwenye Mall au supermarket halafu Kabla ya kuingia aambiwe lipa kwanza kiingilio kwa pesa ndo ukafanye window shopping au ukanunue unachotaka, je hiyo inaingia akilini? Binafsi naona siyo Sawa hata kidogo! Mwenye hoja tofauti aseme!
 
Umeandika ukweli sana !
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom