Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ‘SABASABA’ Ukombozi wa viwanda vya Ngozi nchini

Kagondo

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
296
79
Ngozi zimetumika katika uzalisha wa bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya binadamu, kama vile, viatu, viti mikoba, nguo na mapambo mbalimbali kwa miaka iliyopita kidogo.
0
0


Baadhi ya bidhaa vitokanavyo na ngozi za wanyama.

Viwanda hivyo vya ngozi vimesahaulika kwa muda mrefu na hatima yake kufa kabisa, japokuwa uzalishaji wa wanyama wa kutoa ngozi ambao ni mbuzi, ng’ombe na kondoo wanapatikana.

0


Maonesho ya sabasaba ambayo yamekuwa ni desturi kufanyika kila mwaka , lengo likiwa ni kukuza, kujifunza, na kutoa fursa za biashara kwa wafanyabiashara wa ndani na nje pamoja na wananchi kwa ujumla.

Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanatarajiwa kuanza Juni 28,2016 hadi Julai 8,2016 ambayo yatafunguliwa rasmi Julai 1,2016 na Rais Paul Kagame wa Rwanda, yatakutanisha nchi 30 na jumla ya makampuni 650 ya biashara na huduma za kijamii.

Kutokana na kusudi la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini, maonesha haya ya sabasaba yamelenga kuwa ufunguo wa kutia chachu kwa kuwa tofauti na vile ilivyozoeleka kila mwaka, ambapo imeshauriwa vidhaa za ngozi kuwa nyingi na ikiwezekana kila banda litakalokuwepo katika maonesho hayo liwe na bidhaa yoyote ya ngozi.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa mwaka huu, imekusudia kufufua viwanda vya ngozi kwa njia hiyo, huku ikiwa ni njia mojawapo ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Rais Magufuli katika kufufua viwanda.

Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka amesisitiza suala hilo kwa kutoa wito kwa wananchi na wafanyabiasha wanaopenda kujifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa za ngozi kwani watakuwepo wataalamu kutoka chuo cha ngozi Mwanza watakaofundisha utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na ngozi.
0

Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka akielezea juu ya mafunzo ya utengenezaji bidhaa za ngozi.

Viwanda vyote pamoja na watu wanaojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ngozi, baada ya maonesho haya kuisha watapata fursa ya kuendeleza biashara yao hiyo kwani tayari watakuwa wameunganishwa na wafanyabiashara wengine na kutafutiwa soko kupitia Tantrade.

Ungana na Fikra pevu katika Sababu mbalimbali zinazopelekea kufifia kwa viwanda vya ngozi nchini.

Ubinafsishaji wa viwanda. Viwanda vikikabidhiwa mikononi mwa wengine, hupelekea huvivanya viwanda hivyo kwa jinsiwenyewe wanavyotaka, hii inajumuisha kusafirisha ngozi hizo badala ya kuzalisha bidhaa nchini.

Uchoraji wa alama kweye ngozi za wanyama. Wafugaji wengi hasa wenye mifugo mingi, hutumia alama kama nyenzo ya kuweza kutambua mifugo yao pindi inapoibiwa a kuchanganyikana na mifugo ya watu wengine.

Alama hizo imeshauriwa ziwe zinawekwa sehemu za miguu au vichwani mwa wanyama kama ng’ombe ili kueusha kuharibu ngozi.

Uchinjaji na uchunaji holela. Machinjio mengi ya Ukonga na Vingunguti jijini Dar es salaam, yametajwa kama machinjio korofi ambayo wachinjaji wake hawafuati utaratibu mzuri wa kupata ngozi na badala yake kuharibu ngozi kwa kuhitaji nyama pekee.

Ubora hafifu wa ngozi. Sio kila mg’ombe anafaa kutoa ngozi kwa matumizi ya matengenezo ya bidhaa husika, hivyo basi, mnyama anapaswa kutunzwa vizuri huku akitibiwa magonjwa ya ngozi ili kuifanya ngozi kuwa imara na inayofaa.

Watanzania kwa ujumla hakuna budi kuzichangamkia fursa hii ya kujifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa za ngozi zikiwemo viatu kutoka wataalam watatakaotoka jijini Mwanza chuo cha ngozi.
 
Back
Top Bottom