Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao.......

mimi John Kisekwa..."
Mkuu huyu ni shuhuda au manusura?

Lakini pia umejuaje kwamba huyu mwandishi alikuwemo kweli kwenye hio ferry? Maana sidhani kwa akili za kawaida mtu anusurike ajali kama ile ambapo hata simu yake iliharibika kwa kuingiliwa na maji, leo hii tayari kapata nyingine, (tena kule ukara hakuna duka la smartphone hadi avuke aende Ukerewe) na hapo hapo kapata ujasiri wa kuandika kwenye mitandao eti sijui ni shuhuda?

Nimeona hii post yake kwenye uzi flani nikaipuuza ila wewe naona umeibeba nzima nzima na kuifungulia uzi. Sasa tuthibitishie kuwa kweli yule alikuwemo kwenye ferry.
 
Omnabuzegwe, Unakisia au uko hapo visiwani ?, na kama ndio hivyo how come umbali wa kilometer 50-60 yatumike masaa mawili ?
au ndio kivuko kilikuwa kibovu kinajikokota tu humo majini ?, usafiri wa majini kama ulivyo wa angani unatakiwa for sure chombo kiwe smart, na naamini ifike wakati meli na Vivuko viondolewe chini ya usimamizi wa Sumatra, either wapewe mamlaka ya anga (aviation authority) au kiundwe chombo kingine, waha Sumatra kuna maeneo mengi wameonesha kushindwa kutimiza majukumu yao
Bahati nzuri umenielewa kwamba nilikisia tu
 
Aliyehai naye angenyongwa tu, haiwezekani umeaminiwa wewe na wewe ukajipa ufalme na kumpa mwengine. Jamani tunachezeana sana, ni sawa hizi dala dala za mijini mara nyingi hupewa madeiwaka kuendesha na wao hukaa bar kunywa bia na kulala na wanawake. Hawastahili huruma kwakweli
Kama ile dala dala iliyotumbukia kigongo ferry pale jijini mwanza. Dereva alimpa deiwaka.
 
Katika uokoaji Usalama wa waokoaji ni jambo la kwanza na la msingi.Hivi waokoaji wangeendelea na uokozi usiku wa jana na wao kupoteza maisha si tungeongeza janga juu ya janga.

Naamini uamuzi wa kusitishwa kwa zoezi hilo jana jioni uliangalia vitu vingi na kimojawapo ni uwezekano wa watu kuwa hai masaa karibu 6 chini ya maji na kuendelea kuwa hai.

Kwa waliozoea kuishi karibu na maji mtu anapozama na kumtafuta bila mafanikio mnaacha na kesho yake utamkuta anaelea.

Sidhani kama kuna manusura walikuwa wakionekana in the vicinity of 50m or up to 200m wakitapatapa na wakaachwa.

Wengi wetu tunasema kivuko kimezama karibu na bandari na kilikuwa kinashuhudiwa live sasa tunataka scope ya uokoaji itanuke hadi kenya?
Tupunguze ujuaji tuache siasa za mjitaka.

RIP MAREHEMU WOTE POLENI SANA WAFIWA
Leo kuna mtu katolewa akiwa hai siku ya 3, waite kunguni wenzio wa kijani muweke kikao kujitetea. Halafu Nani alikwambia kwenye maafa cha kwanza ni usalama wa waokoaji? Usidanganye watu hapa.
 
Mongela you need to be proactive.
Ungeanza kujipanga mapema na mahema. Majenereta. Bulbu.fedha kidogo na chakula kwa waokoaji. Huyu aliyeokolewa hai leo angetoka na wengine wengi wasio na hatia.
Mongela alifika eneo na tukio na smart phone minus washauri wake na hakua na mkakati wowote zaidi ya kupigwa picha.
Ulipinga tangu awali, na nilikuunga mkono. Wengine wakasema eti haiwezekani mtu kuwa hai masaa 4 baada ya ajali, Leo MTU katoka akiwa hai baada ya masaa zaidi ya 44! Aibu hii Mingela jiuzulu.
 
Back
Top Bottom