Maombi yangu kwa wahusika wa Julius Nyerere International Airport

Dogo mmoja aliingia na Bonge la Mkasi ndani ya Kibegi cha Mgongoni katika Idara moja nyeti kweli kweli tena sana hapa Dar (Siitaji)
Na kapita kwenye Screening machine,

Chezea Bongo wewe?

Namuuliza uliwezaje kupita nalo?
Nae, ananiuliza, wao walishindwaje kuliona?:oops:

Nikawa nabung'aabung'aa tu.

KIfupi Mswahili atakuwa Mswahili tu vitu vingi vinaendeshwa kwa mazoea.
 
Mbona JKIA kuna check in mbili? Ya chini na ya juu yenye escalator belt, na zote lazima umwage vitu chini. Sasa wewe ilikuwaje hata sielewi.
Unazungumzia terminal ipi mkuu? Mara ya mwisho kusafiri kupitia huko ilikuwa lini ambapo ulitakiwa kumwaga vitu vyako chini?
 
Swali kuu sababu gani unatia vitu vya ncha kali ktk begi lako unaloingia nalo ndani ya ndege wakati ni vitu havistahili kuwepo ndani ya begi lako?

Shukuru watu wa Qatar walikuwa waelewa, ila tusome maangalizo yanayo kataza vimiminika, vitu vya ncha kali au vinavyoweza kutumika kama kifaa cha kuumiza pia tuhakikishe mabegi yetu tunayapakia vitu wenyewe siyo kumuachia mtu akuwekee vitu ambayo hafahamu kuwa vinakatazwa.

Mara kadhaa watu wa usalama airport wanaweza kupitiwa na wasione vitu kama hivyo.
Kupitiwa hakupo, shida ni ubovu wa hizo scanner au scanner kutokutumika.
 
Kumbe hili tatizo bado lipo? Je, shida ni mashine zetu za kuscan ni za viwango vya chini au ni uzembe/kukosa ujuzi kwa wahusika kubaini visivyohusika vilivyomo ndani ya begi wakati wa kuscan?

Nakumbuka miaka kadhaa imepita tulipita hapo na jamaa yangu kuelekea US kupitia Kiwanja cha Schiphol- Uholanzi. Kwenye ukaguzi JNIA tulipita, bila tashwishi yoyote.

Lakini tulipofika Schiphol Inter. Airport, begi la mgongoni la jamaa yangu likaonekana lina kitu kisicho cha kawaida. Hivyo aliwekwa pembeni kwa ukaguzi zaidi na kuulizwa maswali. Akaulizwa kama kuna kitu chochote kisicho cha kawaida amekiweka kwenye begi lake?
Jamaa akakataa katakata. Maswali yalivyozidi, akakasirika. Ikabidi nimpoze jamaa kwamba atulie ili tuone mwisho wake.
Begi likafunguliwa hakukuonekana kitu chochote kisichoruhusiwa. Yule dada (mkaguzi) kwa kuwa alikuwa na hakika kuwa ameona kitu hatarishi kwenye hilo begi, akaanza kupitisha upya kitu kimoja kimoja kwenye scana. Vitu vyote vikapitishwa, kitu kisicho cha kawaida/chenye ncha kali ikaonekana kipo ndani ya shajara (diary). Shajara ikakung'utwa, hatimaye wembe ukodondoka.
Jamaa macho yakamtoka, kwa maana hakumbuki hata huo wembe aliuweka lini ndani ya hiyo diary. Wembe ukachukuliwa na kutupwa kwenye pipa la taka. Na kupewa maelekezo kukagua kwa makini mabegi/mizigo tunayoingia nayo ndani ya ndege ( carry on bags/luggage)
 
Back
Top Bottom