Maombi ya Papa Francis yaliniponya, asema Museveni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Rais Yowei Museveni aliwaambia maelfu ya waumini wa Kikatoliki jana kwamba Papa Francis alimfanya maombi mkono wake ulipovunjika na ukapona.

Museveni ambaye amekuwa rais wa Uganda kwa zaidi ya miaka 30 amesema Papa Francis alimuombea walipokutana New York, Marekani.

“Mkono wangu ulivunjika kwa bahati mbaya nilipogonga kitu na nilipokutana naye (Papa Francis), tulikuwa kwenye chumba kimoja wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN). Nilikuwa narudi kukaa nikitokea kwenye jukwaa baada ya kuhutubia na yeye alikuwa anakwenda kuhutubia, hivyo aliniombea na mkono wangu ukapona,” alisema Museveni hali iliyosababisha waumini kushangilia.

Rais Museveni alitoa ushuhuda huo wakati wa maadhimisho ya Dayosisi ya Kampala kutimiza miaka 50 katika madhabahu ya Kanisa Katoliki Namugongo.

Alisema: “Nakusalimua Kardinali (Fernando Filoni) kutoka Roma. Papa Francis amekuwa rafiki yetu mzuri. Utakumbuka kuwa alikuja hapa kwa maadhimisho ya wafia dini. Jumapili hii ni kilele cha sherehe za mwaka mmoja za Golden Jubilee (miaka 50) katika dayosisi ya Kampala Achini ya kaulimbiu; “Kumbuka, Furahia na Badilika.

Dayosisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1966, imeongozwa na maaskofu Emmanuel Kardinali Nsubuga, Emmanuel Kardinali Wamala na wa sasa ni Dk Lwanga.

Rais Museveni alisema kwamba maadhimisho hayo ya miaka 50 yatumike kumshukuru Mungu kwa kuwalinda Waganda katika kipindi chote cha machafuko katika ya mwaka 1966 na 1986 ambapo watu wapatao 800,000 waliuawa.




mwananchi
 
Back
Top Bottom