Maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo ya corona ya Russia yanazidi kuongezeka

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,869
Lavrov: Maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo ya corona ya Russia yanazidi kuongezeka

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameitaja chanjo ya Sputnik- V kuwa moja ya chanjo bora zilizopo duniani hivi sasa na kusisitiza kuwa, maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo hiyo yanazidi kuongezeka.

Sergei Lavrov amekosoa mwenendo wa Umoja wa Ulaya na kueleza kuwa, muundo wa Umoja wa Ulaya uko kwa namna kwamba hauruhusu kuwepo ushirikiano huru baina ya umoja huo na Russia katika suala la chanjo ya corona.

Lavrov ameongeza kuwa, kwa hali yoyote ile kinachojadiliwa ni kuwa, ni nani atachukua hatua ili kuzuia japo kidogo kuvurugika uhusiano kati ya Moscow na Brussels.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kuwa, leo hii nchi nyingi kama Jamhuri ya Czech zinasubiri kuidhinishwa chanjo ya Sputnik-V na taasisi ya madawa ya Umoja wa Ulaya ili kuweza kuiagiza. Huko Hungary pia hivi sasa wanaifuatilia chanjo hiyo na wametangaza kuwa tayari kuinunua.

Wakati huo huo maombi ya nchi za Ulaya ya kununua chanjo hiyo ya Russia yanazidi kuongezeka. Ni siku kadhaa tu zilizopita pia sisi tulipokea ombi kutoka kwa Mfalme wa Monaco akitaka kupatiwa chanjo jamii nzima ya nchi hiyo ndogo inayopatikana katika pwani ya bahari ya Mediterania.

Wakati huo huo jarida mashuhuri la masuala ya tiba duniani la Lancet lilitangaza katika ripoti yake ya Februari Pili mwaka jana kwamba: chanjo ya Sputnik-V ya Russia ni kati ya chanjo bora na salama zaidi duniani.


My take;
Wakuu hii chanjo ina usalama gani ambao unaweza kutofautiana na wanchi za magharibi?kama lengo na share ya haya makampuni huenda hata hii chanjo ikawa ina share ya umiliki na mabeberu na huenda lao ni moja tu....
 
Ndio Mana naamini Corona was purposely made ili kutengeneza mabilionea wapi Ulaya huko..Imagine tuko Watu bil 7 na kitu dunia nzima.

Sasa hapo chanjo ikipita kea kila mtu ni kiasi gani?
 
Back
Top Bottom