Midavudavu
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 287
- 59
Kijana mmoja wakati wa kijiandaa na mitihani ya kidato cha 4 alikuwa anasoma na wenzake usiku gheto. Huko gheto wenzi wakamfundiosha kuvuta bangi. Bangi ilipomkolea akachanganyikiwa akawa anasema hovyo na kupagawa. Baada ya wenzie kumrudisha kwa wazazi wake ikabidi aitwe mchungaji jirani ili amuombee. wachungaji kama mnavyojua tena akaaanza "toka kwa jina la......na .........hakuna kilichotokea na badala yake jamaa makelele yakazidi. Mmoja kati ya wale aliokuwa anavuta nao bange akashauri "huyu dawa yake nyepesi tu mpeni miwa ale" Ikatafutwa miwa usiku huohuo na jamaa baada ya kufakamia miwa akapata nafuu. Wazazi wakambana jamaa aeleze imekuwaje hadi akajuwa ugonjwa wa mtoto wao unaweza kupona kwa kila miwa. Naye hakuficha " jamani hapa hakuna pepo wala nini sisi tulikuwa tunavuta bange gheto na bahati mbaya jamaa yetu ni mwepesi katika mambo haya". Wazazi angalie makundi ya prep. wanayoshiriki watoto wenu je yanawasaidia au yanachangia kuwaharibu zaidi?. Hili ni tukio la kweli, utani umechukua sehemu ndogo sana.