Maombi ya Maua Sama, Sudi Kadio, Shaffih Dauda na wengine wanne kupata dhamana, kuamuliwa Septemba 24, 2018

Pale usafini walifanya the same tena walikuwa wanazifagia na kukanyaga,
 
Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2018 itasikilizwa Jumatatu Septemba 24, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkaizi Kisutu mbele ya Hakimu Huruma Shaidi

Mbali na Msanii Maua Sama, Watangazaji Sudi Kadio(Soudy Brown) na Shaffih Dauda wengine ni Mshehereshaji Anthony Luvanda, Mpiga picha Michael Mlingwa(MxCarter), Fadhili Kondo na Benedict Kadege

Maua Sama na Sudi Kadio wanadaiwa kushikiliwa kwa kosa la kudhalilisha fedha ya Tanzania kwa kuirusha juu na kuikanyaga

Wengine wanashikiliwa wakidaiwa kumiliki na kuendesha chaneli za YouTube ambazo hazijasajiliwa na TCRA

View attachment 874146
Namuonea uruma sudy tutamis shilawaduu
 
Mbona kwenye matamasha naonaga hata viongozi wakirusha hela jukwaani(kutunza) na zinakanyagwa, lakini sijawahi sikia wakikamatwa. Hizi ndio tunaita double standards. Akifanya huyu ni kosa, lakini akifanya yule sio kosa. Sheria za Tanzania zinabagua.
Mkuu wanachoangalia pale ni maudhui pekee.

Kurusha pesa kutuza au unarusha pesa kukebehi?

Unafyagia pesa baada ya sanduku ulimozihifadhi kuanguka, kupasuka na kusambaa, au unafyagia pesa kuonesha kuwa pesa kwako ni takataka kama ulivyo uchafu mwingine?

Mahakama ndiyo itakayofasiri hilo tendo.
 
Wasifanye double standard wapitie mitandao wasanii wote na wote waliowahi sigina hela kama wao wawachukulie hatua ili kuwaprove wrong kuwa ni bifu kati yao na wakuu wa visasi
Kimsingi kwa utaratibu wa kisheria ukikamatwa wewe basi ndio unatakiwa kujibu mashitaka hivyo utetezi wa mbona flani alifanya hauna mashiko
 
Hiyo inaitwa ni kesi ya kutengenezwa na washitakiwa ili kuvuta attention ya hadhira, kwa ajili ya kiki za pikpiki.

Hivi mishahara ya wafanyakazi ama wasanii, wana pesa za ziada za kuchezea hadi kukufuru?
Baada ya kutiwa huu msukosuko, kamwe hawatarudia kufanya dhihaka ya kitoto kiwango hicho.
 
Back
Top Bottom