Maombi, sala na dua za mke wangu ni kero kwangu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
Nina mwaka wa nane wa ndoa na hakika nimekuwa ni mvumilivu Sana na mwaminifu Sana kwa ndoa yetu.

Nimezaliwa na kukulia kwenye familia ya Kikristo yenye msimamo mkali wa kiimani, hivyo Basi sijawahi kuvuta sigara, kunywa Pombe na hata uzinzi sio mzinzi, mke wangu ni mwanamke pekee kulala naye tangu nizaliwe.

Kinachonikera kwa miaka yote hiyo mke wangu amekuwa akitamani sana kumjua mwanamke ninaye tembea naye nje ya ndoa.

Mara ya Kwanza nikajua ananitania, Mara kwa Mara alikuwa ananiambia darling natamani nimjue mwanamke unayetembea naye, nione kanizidi nini?

Daima jibu langu Mimi nimeokoka siwezi kuwa na mtu mwingine zaidi yako. Haniamini na haamini majibu yangu, simu zangu na e mails yeye ndiye huset password, ana access nazo muda wote.

Sasa kuanzia juzi Yuko kwenye maombi, anaomba aonyeshwe kwa namna yoyote mwanamke ninayetembea naye, maana anachojua yeye hamna mwanaume asiyechepuka.

Mbaya zaidi anaomba kwa kulia kwa sauti huku akipigapiga ukutani.
 
Mimi alikuwa anaomba eti niache pombe nikamwambia hiyo sala yako ikifanikiwa utakufa njaa na watoto hawataenda shule kwani kwenye pombe ndio natengeneza mipango ya pesa!

Na nikamwambia sala zako usiku sana ni kero nitakuwa siji mpaka umalize kwani unanikosesha usingizi .sali mapema au nenda kanisani.

Akafyata mkia kwani nilikuwa ikifika saa sita usiku nampigia kama bado anaendelea na kelele zake za maombi ili niendelee kupika stori sitaki kurudi nikute nyumba imebadirishwa kanisa
 
Sasa kuanzia juzi Yuko kwenye maombi, anaomba aonyeshwe kwa namna yoyote mwanamke ninayetembea naye, maana anachojua yeye hamna mwanaume asiyechepuka.

Mbaya zaidi anaomba kwa kulia kwa sauti huku akipigapiga ukutani
 
Sasa kwa mfano unae huyo mchepuko unamwambia kukuacha hawezi anabaki kufwa kimoyomoyo

Ya nini yote haya kama mwanaume anakucheat muache tu mpaka arobaini yake ifike sio kumchunguza

jamani sisi wanawake bwana unalolitafuta utalipata mwanamke mwenzangu endelea
 
Sasa kuanzia juzi Yuko kwenye maombi, anaomba aonyeshwe kwa namna yoyote mwanamke ninayetembea naye, maana anachojua yeye hamna mwanaume asiyechepuka.
Mbaya zaidi anaomba kwa kulia kwa sauti huku akipigapiga ukutani
Ha ha ha Mshana umesababisha nimecheka hapa kitandani asubhi mpaka naye huyu jamaa yangu kauliza unacheka nini nipe nisome meseji itakuwa imetoka kwa mchepuko nimempa asome ili naye aache kunisumbua na masala yao haya na wanachoudhi zaidi wanapeleka na hela kibao ya sadaka huko wanakotuombea tuwe waume bora eti tuache pombe na tusiwe na michepuko na wakati huu wa mechi za mpira za usiku yaani kabla hujarudi nyumba inakuwa imegeuzwa sinagogi duh duh
 
Sasa kuanzia juzi Yuko kwenye maombi, anaomba aonyeshwe kwa namna yoyote mwanamke ninayetembea naye, maana anachojua yeye hamna mwanaume asiyechepuka.
Mbaya zaidi anaomba kwa kulia kwa sauti huku akipigapiga ukutaniKAKODI PISI KALI MUEL3KEZE HOME AJITAMBULISHE .......ASIMSUMBUE MUNGU ANA MAJUKUMU MAKUBWA KIPINDI HICHI CHA UCHAGUZI ...... MWAMBIE material ya ujenzi yamepanda bei sana ......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom