Maombi kwa Waziri wa Ujenzi wa kumaliza ujenzi wa barabara kutoka Mika mpaka Ruari Port

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mhe.Waziri kwanza nakusalimu. Awali ya yote kwa heshima na taadhima tunakuomba sana kutukamilishia barabara yetu ya kutoka Mika Mpaka Ruari Port mpakani mwa nchi ya Tanzania na Kenya kwa kiwango cha lami Wilayani Rorya.

Matengenezo ya barabara hii yalianza enzi za Ubunge wa Professa Sarungi miaka 15 iliyopita na mpaka sasa kiloimita zipatazo kumi ndizo zimetengenezwa kwa kiwango cha lami kati ya kilomita zipatazo 60.

Tunaye Mbunge wetu na tumemueleza suala hili lakini hakuna utekelezaji, natumaini tujilaumu sisi wenyewe sisi tuliyempa kura. Tunakuomba tena Mhe.Waziri tukamilishie barabara hii kama ilivyoahidiwa na Serikali.

Tunajilaumu sana Prof. Sarungi angeendelea kuwa Mbunge barabara husika ingekwishakamilika.
 
Naamini ujumbe umefika, soon utajibiwa kama alivyofanya prof kabudi kuhusu suala la mikataba ya dharura
 
Back
Top Bottom