Maombi kwa mwaka mpya wa 2021 na shukurani kwa Mungu kwa kutuvusha

Ikulumaliyawananch

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
334
1,000
Maombi ya kuuaga mwaka wa 2020 na kuukaribisha mwaka mpya 2021.

E Mungu Muumba mbingu, nchi na maji. Nakushukuru kwa kuwavusha watanzania wezangu salama katika mwaka wa 2020 na kuwakabidhi mwaka mpya wa 2021. Mungu mwaka ulio upita utufundisha mengi sana ila moja kubwa tulilo kubushwa ni kuwa bado upo wanatawala ulimwengu na unawezo wa kufuta dunia katika sekunde moja. Na kwasababu hiyo wote tulio salimika kuona mwaka huu ni wajibu wetu kumshukuru Mungu na kujirekebisha ili tuendane na matakwa ya Muumba wetu

Mungu na kuomba uwasamehe wote walio husika na wizi wa kura katika uchaguzi Mkuu ulio fanyika October 28,2020 maana Mungu wametenda maovu yasiyo sameheka kwa akili za kibinadamu. kwani kwenda kinyume na matakwa ya ya watu wako ni sawa na kwenda kinyume na amri zako. na anaye kwenda na amri zako anaye weza kumsamehe ni wewe tu. ila Mungu nakuomba wote walio husika na wizi wa kura katika uchaguzi ulio pita kama hawatatubu dhambi hiyo na kujirekebisha, Mungu na kuomba uwape somo takatifu ambaro litawafanya wajutie dhambi hiyo ya wizi wa haki za waja wako.

MUNGU NAKUOMBA ULIANGAZIE MACHO taifa lako la Tanzania kwa kuhakikisha mwaka huu unakuwa mwazo kuibadilisha Tanzania ili iwe na viongozi wanao takona na mapenzi ya watu wako. Maana Mungu kwa miaka ya hivi karibuni taifa hili limeingia mikononi mwa watu wasio ona aibi wala kuogopa kusema uongo mbele ya waja wako na wewe mwenyewe. Mungu kurudisha utawala wa haki katika taifa lako pendwa tanzania.

Mungu na kusihi uliponye taifa hili na ungojwa wa unafiki ambao ndio sasa umekuwa kipimo cha uzalendo. Mungu fungua macho watanzania waweze kuona ukweli na kusimamia ukweli bila woga. Mungu fumbuwa akili za watanzania ili waweze kutumia rasilimali ulizo wapa kwa faida ya watanzania wote kwa usawa na kwa haki.

Taifa limegumbikwa na dhuruma ambayo inaangamiza taifa lako. Mungu kumbusha taifa hili kuwa Somalia iliwahi kuwa taifa lenye uchumi mkubwa dunia lakini dhuruma na ubaguzi ndio vilivyo ifikisha hapo ilipo , kwa maana hiyo hata Tanzania haina kinga wala haina mkataba na Mungu wakuepusha yaliyo ikumba Somalia,Somalia,liberia, Libya na mataifa mengine. Mungu nakuomba lekebisha watu wako kabla hawajaangamia

Mungu nakuomba wape maarifa watanzania waweze kushinda janga la coronavirus maana Mungu wengi wameangamia kwa kukosa maarifa na kuukana ukweli wako

Mungu Jina lako lihimidiwe na Viumbe wote, nakusihi Mungu ulilinde taifa lako la Tanzania katika mwaka huu wa 2021. Mungu na kuomba uwaumbuwa viongozi wote wa dini ambao wamegeuza mafundisho yako kama njia ya kuwalaghai waja wako wenye shida. Mungu nakuomba uwape akili watanzania waweze kuebuka utapeli wa kiimani ambao umeshamili katika taifa lako katika miaka ya hivi karibuni

Mungu na kuomba viongozi wote wa kisiasa watakao iba mali za waja wako uwape adhabu kali itakayo kuwa fuzo kwa wezi wote. Mungu na kuomba wanafunzi wote watakao jaribu kuiba mitihani badala ya kusoma kwa bdii na kuelewa Mungu uwape adhabu ya kuwa ombaomba kwa miaka miwili katika maisha yao. pia Mungu na kuomba walimu wote watakao vujisha mitihani au kuomba rushwa ya ngono Mungu wape ulemavu wa kukosa nguvu za kiume maisha yao yote. Mungu pia na kuomba polisi wate watakao omba rushwa barabarani Uwape adhabu ya ya kufukuzwa kazi ili wakajiajiri waona mateso walio waomba rushwa.

Mungu na kuomba mwaka huu uwe wa haki na atakaye tumia cheo chake kudhurumu haki ya mtu yoyote umpe adhabu inayo sitahili kuligana na utakavyo pendezwa. Mungu nakuomba wafanya bishara wote watakao tumia ujaja kujipatia faida kwa njia za udanganyifu Mungu filisi wote wakaanze upya kwa kuzingatia haki. Mungu nakusihi uwabariki sana wakulima na wafugaji na wote wanao fanya kazi zao kwa uadilifu.

Mwisho Mungu nakuomba uwalinde na uwabaliki watu wote walio patwa na majanga mengi katika mwaka ulipita kwa sababu ya kutetea haki na usawa katika taifa lako pendwa la Tanzania. Mungu namalinzia kwa kusema asante maana nakumbuka mengi mazuri namengine sio mazuru sana kwa akili zangu ambayo umenitendea katika mwaka huu wa 2020. MUNGU KAMA UTANIPA UZIMA KUONA MWAKA MWINGINE NITARUDI KUKUSHUKURU KWA YOTE UTAKAYO TENDA NA YALE UTAKAYO ACHA. Mungu mbali yoyote akaye soma haya maombi na kuyafanyia kazi. Amina.
 

My Sons Legacy

JF-Expert Member
Feb 4, 2019
2,650
2,000
Amiiin
Ubarikiwe sana ndugu mtanzania mwenzetu kwa maombi haya

Sema hujaandika hata aya moja umefaa kushuka tuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom