Maombi gani ya watu wako wa karibu yanakukera? Ukiachilia mbali pesa?

Walt white

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
236
591
Wakuu, tukiachana na watu wako wa karibu kukuomba pesa kipi kingine ukiombwa huwa unakereka sana? Binafsi ni haya matatu.

1.Simu yako ina dakika uniazime?
2.Kuombana vifaa vya kazi.
3.Kuombana mavazi hasa viatu.

Je wewe kuna mengine yanakukera au yote ni sawa kwako?
 
Wakuu, tukiachana na watu wako wa karibu kukuomba pesa kipi kingine ukiombwa huwa unakereka sana? Binafsi ni haya matatu
1. Simu yako ina dakika uniazime?
2.kuombana vifaa vya kazi
3.kuombana mavazi hasa viatu.
Je wewe kuna mengine yanakukera au yote ni sawa kwako?
Kuna kaharufu ka-uchoyo hapa, si vizuri kunyimana vilivyo ndani ya uwezo.
 
Mimi siazimani nguo wala viatu kabisa.
Hata nyumbani kwetu Mama yangu alikuwa hataki tabia ya kuvaliana hata kama ni ndugu kwahiyo nikajifunza sio tabia nzuri pia mtu akivaa halafu uvae tena inatia kinyaa.
Kipindi nasoma kuna bidada alikuwa anapenda kuazima halafu ni rafiki siku moja akaniazima viatu nikashindwa kumnyima.Alivyorudisha vimekuwa vikubwa nikivaa vinanipwaya ikabidi nimuachia huku roho imauma.
Toka siku hiyo nimekoma hata kama ni shosti kiasi gani.
Ila hii tabia tunayo sana wanawake.
Mtu anaazima hadi vyombo akipata wageni na uwezo wakunua anao ila atakumbuka kusuka na kuvaa vizuri ila vya muhimu hapana.
Bora basi arudishe vikiwa katika hali nzuri utarudishiwa kimeharibika au kina kasoro.
Kuna watu hawaoni tabu ataazima hata kila siku hata kama hicho kitu ana uwezo wa kukinunua lakini ataazima tu.
 
Back
Top Bottom