Baba V
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 19,482
- 9,517
Eee Baba yetu uliye mahali pa juu palipoinuka, Ninakuja mbele zako kwa moyo wa ukunjufu, ninaukaribisha uwepo wako mahali hapa,ninakaribisha upendo wako mkuu utamalaki katika jukwaa hili, ninaomba roho yako itawale mahali hapa,ninaomba upendo wako ulio mkuu upandikize mbegu ya upendo katika mioyo ya wana chit chat wote na Jf kwa ujumla,Ninakwenda kinyume na nguvu za giza,ninavunjavunja nguvu za mwovu ibilisi, ninaliangamiza pepo la ukuwadi,ninaziangamiza nguvu za mapepo ya kupenda wake na waume za watu, ninavurugavuruga mipango ya kuvunja ndoa za watu, ninakwenda kinyume na pepo la UZUSHI na kuchafua majina ya watu, ninakemea pepo wa tamaa ya pesa na mitoko ya weekend isiyo na tija, ninavunjavunja pepo linalojiinua la kukosekana kwa uaminifu na cheating, ninaua kabisa pepo la talaka na vipigo katika ndoa ASHAGHALABABOSSIKAAALATASAA, Ninaziombea kamati zote ikiwapo yangu ya maombezi ziweze kufanya kazi kwa uaminifu na wepesi, Ninamuombea Mwenyekiti wa tume yetu Baba V, umpe busara katika utekelezaji wa majukumu yake na kuzisimamia kamati zote, umuepushe na chuki binafsi bali atende kazi kwa manufaa ya wote, kwa ukuu wako ninaikabidhi chit chat mikononi mwako. AMEN
Last edited by a moderator: