Habari zilizopo hivi sasa ni kuwa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wametinga ofisi za gazeti la Mawio zilizopo Magomeni Mwembe Chai mchana huu kumtafuta mhariri na Mkurugenzi Mkuu wa Mawio, SIMON MKINA.
Lakini hawakufanikiwa kumkuta ila kwa habari zilizokuwepo mhariri huyo yupo Polisi amejisalimisha toka asubuhi lakini maofisa hao hawakuishia hapo, walifunga safari mpaka kwenye ofisi ya gazeti la MWANAHALISI zilizopo Kinondoni vijana kwa nia ya kwenda kumtafuta mhariri huyo napo hawakufanikiwa kumkuta.
==================
UPDATE
Wahariri wa Mawio wajisalimisha Polisi
Mhariri mtendaji wa Mawio, Simon Mkina na Mhariri Jabir Idrissa wamejisalimisha polisi, wamehojiwa chini ya Mwanasheria wao Fredrick Kihwelo.
Wahariri walijisalimisha polisi saa 9 jioni na kuanza kuhojiwa mpaka muda wa jioni walipomaliza. lakini wamenyimwa dhamana na leo tarehe 19 watafikishwa mahakamani.