Maofisa wa JWTZ kuhusishwa na fedha za Uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi

Huwezi pewa iyo list unless inchi ikiiomba sasa waliomo kwenye list ndio wenye inchi what do you expect?
 
Umesema kweli kabisa! Hatutaki usanii kwa jambo kubwa kama hili. Wakati mamilioni ya wa-TZ, wanaishi kwa kula mlo mmoja kwa siku, hawa wenzetu wachache wanaogelea kwenye utajiri wa kutisha kwa kuwekewa mabilioni ya shilingi, kama rushwa kwenye mabenki hayo ya uswisi, na kampuni za kigeni zinazochimba mafuta na gesi.

Kwa bahati mbaya sana, hiyo list ya waliowekewa hizo pesa, itakuwa jambo lisilowezekana kutangazwa na serikali hii ya CCM. Kwa kuwa inahusisha watu wenye madaraka makubwa sana kwenye serikali ya awamu hii na iliyopita. Kwa uchache tu miongoni ya majina hayo ni JK, Mkapa, Hosea, Lowasa, Mwema, Chagonja,Shimbo, Membe,Balali na Mkulo!!

Sasa kwa list hiyo ni wazi juhudi zote zitafanywa na serikali ya CCM, hadi mwisho wa Dunia, kuhakikisha list hiyo haijulikani kwa walalahoi wa nchi hii, maana ikitolewa rasmi ripoti hiyo kwa wananchi, maana yake huo ndiyo utakuwa mwisho rasmi wa chama cha magamba!!

Asante mkuu kwa kifunguka. Eti wakajifanya Balali alikufa kumbe waliweka gogo kwenye jeneza!! Kweli Tanzania kirusi hatari!!!
 
Kwakushirikiana na mashirika ya kijasusi ya CIA-
USA, M1-6-UK, RAW-India, DGSE-Ufaransa, FSB
Urusi, ISI Pakistan, na MSS-China, ambayo
yamekuwa yakifuatilia nyendo za fedha haramu
hasa za kighaidi dunia, tumefanikiwa kutambua
Watanzania, Wakenya, Waafrika kusini, Waganda na
Wakongo wengi matajiri walioficha fedha uswisi.
Hapa nitawaorodhesha Watanzania tu;
Orodha ni ndefu ila hapa ni wale walioficha zaidi
ya USD $3.5 mmilion kila moja. Wamo wanasiasa
pamoja na wafanyabiashara kadhaa maarufu.
Imebainikwa kwamba fedha nyingi za wanasiasa
zimewekwa na makampuni ya nje yenye shughuli
Tanzania. Wamo hata Makatibu Wakuu Wizarani
na wakurugenzi ila hawajafikia USD3.5million ndio
maana majina yao hayamo.
Orodha kamili ni:
Jakaya M. Kikwete, January Makamba, Abdalla
Kighoda, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Andrew
Chenge, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Rostam
Aziz, Yusuf Manji, Ridhiwani Kikwete, Mohamed
Dewji, Bernard Membe, Paul Chagonja , Zitto
Kabwe, William B. Mkapa, Said Mwema,
Abdulrahman Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S
Balali, Basil Mramba,Mustapha Mkullo, Grey
Mgonja, Patrick Rutabanzibwa,Tanil Somaiya, Jeetu
Patel, Onoko Okesukwu mwenye asili ya Kinigeria,
Awadh Mohamed (mwenye uraia wa msomalia) na
Subhash Patel
Orodha ya wanaoingiza pesa chafu/haramu na
kuzitakatisha ni ndefu nitawawataja

VIGOGO 10 wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).

Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).

Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.

Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: “Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge.”

“Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?.”
Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.

“Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi,” alisema Zitto.

Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.

Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.

Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi.

“Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti ambazo zinamilikiwa na wanasiasa wakubwa nchini na wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini,” kilidokeza chanzo hicho.

Kugundulika kwa kiasi hicho cha fedha katika benki za Uswisi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB) iliyotolewa mwaka huu.
 
Hii nchi kwa kweli hakuna utawala bora kabisa na ndio maana mpaka kiongozi mkuu wa inji nae yumo humo ndani.
 
No.. No... No, I am he not she!! Hahaaaha mkuu nitaitoa usijali.

Sawa mkuu umefanya vyema. Unajua avatar inawakilisha gender ya mtu pia. Ukiweka picha ya kike inawalisha "she" na ukiweka cha kiume inawakilisha "he". Ngoja sasa na mimi nii-edit post yangu niliyosema "mrembo" nisamehe mkuu kwa hilo.
 
Taarifa ya kuwepo maafisa watatu wastaafu wa JWTZ katika orodha ya vigogo walioficha fedha uswisi ni pigo kubwa sana kwa nchi kwani hii taasisi ni moja ya taasisi ambazo Watanzania tulikuwa na imani nayo bado lakini pia linaweza kuwa pigo kwa nchi kwani inawezekana kabisa hali ya jeshi letu kivifaa sio nzuri sana kwani kuna uwezekano pesa za kununulia vifaa/Silaha zilichakachuliwa na hivyo aidha hatuna silaha nzuri na za kutosha au tuna silaha duni/zilichochakachuliwa.

Kama tulivyoona ajali kadhaa ya choppers cha jeshi zinazoaminika tuliuziwa zikiwa zimeshachoka lakini inawezekana pia hela hizo zilizofichwa uswisi ni matokeo ya kudhulimiwa kwa wapiganaji wetu na hivyo kuua morali ya vijana wetu.

Kwangu kuwepo kwenye orodha hii maafisa nyeti na wanaopaswa kuwa na uzalendo wa hali ya juu hata kujitolea maisha yao kutulinda ni Pigo kubwa sana kwa nchi yetu.
Kama katiki list ya wastaafu hayumo General Mboma list hiyo itakuwa feki.
 
Tunataka majina wala sio mbwembwe maana hizi stori kila siku hatuzitaki kikubwa taja wahusika ili tuwafuatilia kwa kila hali
 
Yangu Macho.
Haya endelea kuwachokonoa Wanajeshi.
Siku wakifunguka mie simo.
Hili sio eneo la kuchezea.
 
isije ikawa ni bra bra za kila siku kila mtu akiibuka nina orodha

Kuna ile link ya Ugiriki kama umeiona hapo mwanzoni. Kila mtu anasema ana majina wengine kwenye CD, wengine kenye USB flash drive.

Kazi kweli kweli
 
Kumbe kuipata hiyo list siyo ngumu wala nini. Dawa ni kuwasiliana na waziri wa fedha wa Ufaransa tu
 
Yangu Macho.
Haya endelea kuwachokonoa Wanajeshi.
Siku wakifunguka mie simo.
Hili sio eneo la kuchezea.
Kenge,
Inabidi tuwachokonoe hadi wajue kuwa hawapati maslahi bora kwa sababu wakubwa wachache wanapora mali ya taifa. Wakifanya uasi tunaweza kupona.

Nilijua kuwa hata wao wamechoka pale askari wa cheo cha chini alipotoa maoni kwenye tume ya katiba, tena mbele ya maofisa wake bila woga, kuwa mafisadi hukumu yao iwe kifo, na mafisadi jeshini wauawe kwa risasi tena hadharani. Hayo ndiyo yalikuwa maoni yake kwa katiba mpya. Hata wao wamechoka. Wanaofaidi ni kundi dogo sana huko jeshini.
 
Sawa mkuu umefanya vyema. Unajua avatar inawakilisha gender ya mtu pia. Ukiweka picha ya kike inawalisha "she" na ukiweka cha kiume inawakilisha "he". Ngoja sasa na mimi nii-edit post yangu niliyosema "mrembo" nisamehe mkuu kwa hilo.
Usijali mkuu!! Tuendelee tu na mjadala wetu wa JWTZ na wizi wa kutupwa.
 
Majina yao haya hapa

Jakaya M. Kikwete, January Makamba, Abdalla Kighoda, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Manji, Ridhiwani Kikwete, Mohamed Dewji, Bernard Membe, Paul Chagonja , William B. Mkapa, Said Mwema, Abdulrahman Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S Balali, Basil Mramba,Mustapha Mkullo, Grey Mgonja, Patrick Rutabanzibwa,Tanil Somaiya, Jeetu Patel, Onoko Okesukwu mwenye asili ya Kinigeria, Awadh Mohamed (mwenye uraia wa msomalia) na Subhash Patel

Lowassa mbona simuoni hapo??list haijakamilika iyo.
 
Kenge,
Inabidi tuwachokonoe hadi wajue kuwa hawapati maslahi bora kwa sababu wakubwa wachache wanapora mali ya taifa. Wakifanya uasi tunaweza kupona.

Nilijua kuwa hata wao wamechoka pale askari wa cheo cha chini alipotoa maoni kwenye tume ya katiba, tena mbele ya maofisa wake bila woga, kuwa mafisadi hukumu yao iwe kifo, na mafisadi jeshini wauawe kwa risasi tena hadharani. Hayo ndiyo yalikuwa maoni yake kwa katiba mpya. Hata wao wamechoka. Wanaofaidi ni kundi dogo sana huko jeshini.

Hapa umenena mkuu
 
Back
Top Bottom