BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Maofisa ubalozi wanawanyanyasa Watanzania
JIBU LA SWALI LA MBUNGE KIGOMA KASKAZINI
na Peter Nyanje na Rachael Chizoza, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
WATANZANIA wengi walioko nje ya nchi hawaoni umuhimu wa kwenda kujiandikisha katika ofisi za balozi kutokana na manyanyaso wanayoyapata kutoka katika ofisi hizo, Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya alisema jana.
Akiuliza swali la nyongeza, Sakaya alisema kuwa balozi nyingi haziwajali Watanzania wanaoishi nje katika maeneo yao kiasi kwamba hawaoni umuhimu wa kwenda ubalozini kujiandikisha.
Aliutaja ubalozi wa Canada kama mfano wa balozi ambazo haziwajali Watanzania na kuihoji serikali inachukua hatua gani kurekebisha hali hiyo.
Katika swali la msingi, Kabwe Zitto (CHADEMA) alihoji serikali ina mpango gani wa kuwa na maofisa maalum wa kushughulikia masuala ya jumuiya za Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Katika swali la nyongeza, Zitto alisema balozi kadhaa haziwajali Watanzania wanaoishi nje na kutolea mfano wa vifo vya Watanzania wawili waliouawa Michigan, Marekani zaidi ya mwaka mmoja uliopita, lakini hadi sasa ubalozi haujaonyesha juhudi zozote za kuwasaka waliofanya mauaji hayo.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Idd, alisema iwapo kuna balozi zinazowanyanyasa Watanzania, zinakwenda kinyume cha majukumu yake.
Alisema kazi kubwa ya balozi hizo ni kulinda maslahi ya Watanzania walioko kwenye nchi hizo kwani zinahesabika kama sehemu ya Tanzania katika nchi ziliko.
Aidha, Naibu Waziri huyo alikubaliana na Zitto kuwa jumuiya za Watanzania wanaoishi nje ya nchi, zinaongezeka kutokana na kukua kwa mahusiano baina ya Tanzania na nchi nyingine kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Alisema kila Mtanzania anayekwenda nje ya nchi anatakiwa kwenda kujiandikisha katika ofisi ya ubalozi ulio karibu na kutoa taarifa zake ili kuwawezesha maofisa wa ubalozi kujua yuko wapi na shughuli zipi.
Naibu Waziri huyo alisema kutokana na ongezeko la Watanzania katika baadhi ya nchi, hivi karibuni wizara ilichukua hatua ya kupeleka maofisa uhamiaji katika balozi kama vile London, Washington, Nairobi, Pretoria, Bujumbura na Abu Dhabi.
Alisema tatizo lipo kwa Watanzania wanaoingia katika nchi hizo isivyo halali kwa kuwa wahamiaji wa aina hii hawapeleki taarifa zao ubalozini, hivyo kuwa vigumu kuwapatia huduma za kijamii kupitia balozi hizo.