MANYONI: Mwanamke afariki baada ya kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua kwenye duka la dawa

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
FB_IMG_1485449309053.jpg

Mama moja wa kijiji cha Lulwangwa halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni amepoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi baada ya yeye na mume wake kuamua kwenda kujifungulia kwenye duka la dawa ambalo halikusajiliwa na aliyetoa huduma hiyo hana ujuzi wa kuzalisha.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu mganga wa halmashauri ya Itigi Daktari Zuberi Hamisi Abdalah amesema pamoja na kwamba uchunguzi bado unaendelea ,lakini mama aliyefariki ametambulika kwa jina la Helena Maduhu aliyekwenda kwenye duka la dawa kwa ajili ya kujifungua baada ya kuambiwa na muuguzi wa zahanati ya Itagata aende hospitali ya Itigi baada ya wao kushindwa.

Akieleza mume wa marehemu bwana bahame kanuda amesema yeye baada ya kuambiwa ampeleke mke wake katika hospita kubwa alikutana na bwana shingu hengwe ambaye ana duka la dawa na kumwomba kumsaidia kumzalisha mkewe .

Bwana Shingu Hengwe anayedaiwa kumzalisha mama huyo katika duka lake la dawa,baada ya mzazi kufariki aliamua kumsafirisha marehemu na pikipiki wakiwa na mumewake kumpeleka kijijini kwao, pikipiki ikaisha mafuta na yeye alitoweka na kutafutwa zaidi ya saa nne kabla ya kukamatwa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Itigi ambaye aliamua kusimamia shwala hilo ilimlazimu kutuma watu umbali wa zaidi ya kilomita kumina tano ambapo marehemu alipo jifungulia kwenye duka la dawa na kukukuta mtoto aliyezaliwa akiwa mzima kafungiwa ndani ya nyumba akilia huku wenye nyumba hawapo.

Chanzo: ITV
 
Yaani hasingenunua ndege ndio watanzania wasingefariki? Sijakuelewa unachoongelea.

Update: aliporusha uzi huu aliuleta wa kudai manunuzi ya ndege... juu ya kifo kilichotokea. Now habari inaeleweka kweli inasikitisha.
 
Yaani hasingenunua ndege ndio watanzania wasingefariki? Sijakuelewa unachoongelea.
Mama amejifungulia kwenye duka la dawa kwa sababu dawa hazipo hospitalini.
Dawa zingenunuliwa za kutosha na kusambazwa hospitalini, wanaojifungua wangewahishiwa huduma. Angewahishiwa huduma huenda wangeokoa maisha yake
 
Mungu atusaidie aisee maisha yakina mama wajawazito yapo hatarini sana na sio kipaumbele cha serikali...haya matatizo ya Nchi masikini haya...
 
Unadhani kapenda?Angepatiwa huduma kwenye hiyo Zahanati hayo yangetokea?Umewahi ona jinsi mwanamke mwenye uchungu anavyovuja damu?
Rafiki ninajua sana haya mambo kuliko unavyofikili,wakati mwingine twaweza kua na matatizo cc wananchi na watu wanakimbilia kuanza siasa na lawama kwa serikali,hata kama iko na makosa lakini kwenye udhaifu wa mtu kama mtu au kutokuelewa kunaonekana,nimekua kwenye mashirika na kufanya kazi huko katika jamii hasa vijijini,ninaelewa sana wananchi tukoje.swala la kufikia kujifungua na mtu hajaenda kituo cha afya mpaka uchungu unampata ni swala la yeye na mume.sisi sote tuna wake na tunawatoto tunajua,huko vijijini ktk zahanati pamoja na madhaifu hata yawepo lakini elimu hii hutolewa kwa wamama wajawazito,tena huambiwa waende na waume zao clinic na wanaume hua wabishi kwa wake zao,mimi si mtu wa Afya lakini nimetumika ktk shirika lenye kutoa misaada huko ktk Zahanati,mashule na maendeleo mengine ya jamii,umesema sawa lakini si sawa kwa habari iliyopo hapa ya mama na mumewe mpaka siku za kujifungua hawazijui,wamechelewa na kujikuta wanaingia duka la madawa.hapa pana shida kwa marehemu na mumewe.japo ni jambo la kusikitisha na MUNGU amlaze mahala pema lakini huo ndio ukweli.
 
Pole nyingi kwa Mume wa marehem....mi nadhani tatizo ni kipato,huyo mume wa marehem angekua na pesa angeweza kuokoa maisha ya mkewe,ila ndio hivyo tena vijijini wengi wanategemea kilimo na ufugaji,sasa na hii hali ya ukame tutegemee kusikia taarifa kama hizo.
 
Hapa kwa uelewa wangu mdogo ni elimu, hawa wanandoa wangekuwa na elimu na uelewa wa kutosha kuhusu uzazi wasingeenda duka la dawa baridi kujifungulia, inaonekana hata kliniki hawajahudhuria hata mara moja,
 
Rafiki ninajua sana haya mambo kuliko unavyofikili,wakati mwingine twaweza kua na matatizo cc wananchi na watu wanakimbilia kuanza siasa na lawama kwa serikali,hata kama iko na makosa lakini kwenye udhaifu wa mtu kama mtu au kutokuelewa kunaonekana,nimekua kwenye mashirika na kufanya kazi huko katika jamii hasa vijijini,ninaelewa sana wananchi tukoje.swala la kufikia kujifungua na mtu hajaenda kituo cha afya mpaka uchungu unampata ni swala la yeye na mume.sisi sote tuna wake na tunawatoto tunajua,huko vijijini ktk zahanati pamoja na madhaifu hata yawepo lakini elimu hii hutolewa kwa wamama wajawazito,tena huambiwa waende na waume zao clinic na wanaume hua wabishi kwa wake zao,mimi si mtu wa Afya lakini nimetumika ktk shirika lenye kutoa misaada huko ktk Zahanati,mashule na maendeleo mengine ya jamii,umesema sawa lakini si sawa kwa habari iliyopo hapa ya mama na mumewe mpaka siku za kujifungua hawazijui,wamechelewa na kujikuta wanaingia duka la madawa.hapa pana shida kwa marehemu na mumewe.japo ni jambo la kusikitisha na MUNGU amlaze mahala pema lakini huo ndio ukweli.
Nina wasiwas na Elim yako nahizo kaz zko, umeambiw aliend zahanat akaambiw akapewa rufaa aende zahanat ya juu kutokana madakatar wameshndw naon unatoa povu la kaz zako tu
 
Nina wasiwas na Elim yako nahizo kaz zko, umeambiw aliend zahanat akaambiw akapewa rufaa aende zahanat ya juu kutokana madakatar wameshndw naon unatoa povu la kaz zako tu
Unazungumzia elimu?hata mimi na wasi wasi na elimu yako,unayo kidogo lakini hauna pesa,so unataka kuchanganyikiwa,unazungumza elimu?we upo nayo?hebu rudia kusoma maandishi uliyoweka hapa
 
Back
Top Bottom