Manyerere aachia ngazi Mtanzania

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti la Mtanzania, manyerere Kacton amejiuzulu. Mpaka sasa sijapata habari za wazi kwa nini amechukua nafasi hiyo lakini ni dhahiri kuwa hatua yake italeta mabadiliko katika kampuni hiyo inayomiliki magazeti kadhaa.
Pia, inaweza kuwa njia ya kumhamisha kutoka hapo alipo na kumpeleka kuimarisha magazeti mengine ambayo yana maslahi na mabosi wake wa sasa
 
Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
638
41
Kwani Magazeti Ya Mtanzania Yanamilikiwa Na Nani? Halafu Mbona Gazeti La Rai Siku Hizi Ovyo Sana.
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
520
Aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti la Mtanzania, manyerere Kacton amejiuzulu. Mpaka sasa sijapata habari za wazi kwa nini amechukua nafasi hiyo lakini ni dhahiri kuwa hatua yake italeta mabadiliko katika kampuni hiyo inayomiliki magazeti kadhaa.
Pia, inaweza kuwa njia ya kumhamisha kutoka hapo alipo na kumpeleka kuimarisha magazeti mengine ambayo yana maslahi na mabosi wake wa sasa

Mpitia Njia, wewe pita na lwako tu. Unategemea mabadiliko gani kutoka New Habari Cooperation? Nadhani hiyo Kampuni ina-survive kwa ruzuku tu za Mmliki wake, ukweli ni kuwa yamepoteza Wateja sana mimi nikiwa mmojawao.

Kwani NHC ina magazeti gani mengineyo zaidi ya Mtanzania, Rai, The African, Dimba na Bingwa? Hili la Bingwa sijui kama bado lipo maana silioni siku hizi. Zamani nilikuwa sikosi Dimba Jumapili na Rai Alhamisi lakini sasa hata hayanivutii tena.
 
Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
638
41
mpitia Njia, Wewe Pita Na Lwako Tu. Unategemea Mabadiliko Gani Kutoka New Habari Cooperation? Nadhani Hiyo Kampuni Ina-survive Kwa Ruzuku Tu Za Mmliki Wake, Ukweli Ni Kuwa Yamepoteza Wateja Sana Mimi Nikiwa Mmojawao.

Kwani Nhc Ina Magazeti Gani Mengineyo Zaidi Ya Mtanzania, Rai, The African, Dimba Na Bingwa? Hili La Bingwa Sijui Kama Bado Lipo Maana Silioni Siku Hizi. Zamani Nilikuwa Sikosi Dimba Jumapili Na Rai Alhamisi Lakini Sasa Hata Hayanivutii Tena.

Thanks Ibrah Umenijbu Kiaina Huyo Mfadhili Kazi Yake Ni Kua Vyombo Vya Habari Kila Anacho Gusa Kinakufa Amelaaniwa
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Mpitia Njia, wewe pita na lwako tu. Unategemea mabadiliko gani kutoka New Habari Cooperation? Nadhani hiyo Kampuni ina-survive kwa ruzuku tu za Mmliki wake, ukweli ni kuwa yamepoteza Wateja sana mimi nikiwa mmojawao.

Kwani NHC ina magazeti gani mengineyo zaidi ya Mtanzania, Rai, The African, Dimba na Bingwa? Hili la Bingwa sijui kama bado lipo maana silioni siku hizi. Zamani nilikuwa sikosi Dimba Jumapili na Rai Alhamisi lakini sasa hata hayanivutii tena.

Mabadiliko niliyoyasema, kwa kuangalia haraka haraka ni yale ya kawaida ya kumpata mtu wa kuziba nafasi yake.
Lakini ukiamua kurudi nyuma kidogo na kudurusu, unaweza kuhusisha na mtikisiko ambao kampuni hiyo imeupitia katika siku za hivi karibuni na kusababisha mabadiliko yaliyowaondoa baadhi ya wahariri kama Muhingo ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Balile katika Rai.
 
Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
638
41
Manyerere Aje Ukumbini Atuambie Mambo Yanakwendaje,pia Naona Watu Waliokuwa Royal Kwa Ulimwengu Wanaondoka,kwani Rai Sasa Imedolola Kama Uhuru Na Mzarendo
 
Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
255
Manyerere Aje Ukumbini Atuambie Mambo Yanakwendaje,pia Naona Watu Waliokuwa Royal Kwa Ulimwengu Wanaondoka,kwani Rai Sasa Imedolola Kama Uhuru Na Mzarendo

Kweli naungana nawe PEZZONOVANTE aje hapa mwenyewe atueleze maana nasikia anajiandaa kuwa DC wa Rorya wilaya mpya kule Tarime.
 
Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,775
2,712
Hakika aje mwenyewe aseme, isije ikawa alikataa kitita kwa ajili ya kuwaosha Mafisadi. Akapewa option.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,925
10,426
Hizi habari kuwa amepewa kazi kwenye magazeti mapya yanayotegemewa kutoka....ajili kuwasafisha mafisadi ...nahisi soon mtamsikia kwenye magazeti mapya ya mafisadi kwa ahadi ya donge nono.....labda nae ameona mbali kama Salva....alivyoona...
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Na mwananchi nako nasikia watu kama sita hivi wanaachia ngazi leo. Kuna habari kuwa wanakwenda The Guardian Ltd. Kama kuna mwenye habari zaidi, please atuhabarishe
 
Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
638
41
hizi Habari Kuwa Amepewa Kazi Kwenye Magazeti Mapya Yanayotegemewa Kutoka....ajili Kuwasafisha Mafisadi ...nahisi Soon Mtamsikia Kwenye Magazeti Mapya Ya Mafisadi Kwa Ahadi Ya Donge Nono.....labda Nae Ameona Mbali Kama Salva....alivyoona...

Duu Ugali Unawageuza Watu Bwana Salva Shujaa Wetu Leo Nyimbo Anazoimba Vichekesho Duu Umasikini Mbaya Sana.
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Watu wengi wa Mwananchi wanakimbilia IPP Media,na sijui tatizo liko wapi?Sakina datoo alishaondoka zamani tu.Labda maslahi.

Mwanakijiji alishwahi kusita kuandikia gazeti Moja..atakuwa anajua zaidi what is driving waandishi kukimbia na kuhama magazeti,

kuna nafasi iko wazi sehemu..........
 
Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,576
1,090
Hakika aje mwenyewe aseme, isije ikawa alikataa kitita kwa ajili ya kuwaosha Mafisadi. Akapewa option.

Hiyo sikubaliani na wewe, huyu jamaa hawezi kataa kitita kwani ndicho kilichomuweka mtanzania, Kazi yake ilikuwa na kuwaosha sasa labla kaona taaluma inakuwa impaired.
 
Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
255
Na mwananchi nako nasikia watu kama sita hivi wanaachia ngazi leo. Kuna habari kuwa wanakwenda The Guardian Ltd. Kama kuna mwenye habari zaidi, please atuhabarishe

Ni kweli kuna taarifa za watu kutimua pia mwananchi lakini mpaka jana aliyethibitika kuhama ni Richard Mgamba tu ambaye ametimkia The Guardian ingwa orodha imewataja watu wengi. huyu mgamba inasemekana amemfuata swahiba wake Datoo ambaye ndiyer amekuwa akisuka mpango wa kuwaondoa na wengine Mwananchi hasa lengo likiwa ni Kuibomoa The Citizen.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom