Manyaunyau apewa kibali cha kuagua na serikali na polisi je nchi inaamini uchawi?

king11

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
327
79
Wakati wa kuelekea uandikwaji wa katiba mpya, katika karne ya 21 bado taifa linafikia wakati wa kutoa kibari kwa waganga wa kienyeji kupita ndani ya nyumba za watu kusaka uchawai na irizi, hii ni picha ya wazi jinsi taifa lilivyopoteza uelekeo na kutumia muda mwingi katika kupambana na uchawi badala ya kukuza uchumi.

Katika wilaya ya ilala kata ya ukonga serikali imetoa kibari kwa mganga wa kienyeji aitwaye manyaunyau kutafuta wachawi wote katika kata hii, je hivi ndivyo vipaombele vya serikali yetu?

kama hiv ndivyo vipaombele basi kwenye katiba mpya tuweke sheria ya uchawi na serikali ikubali matumizi yake na kuingiza katika nyenzo za serikali,
 
Mkuu hujui kuwa wachawi na waganga wa kienyeji wana ushawishi mkubwa katika nchi hii? Wananchi wengi wa nchi hii wanapiga ramli na kuaguliwa na hao wataalam. Hukuona Babu alivyopewa baraka zote wakati ule wa msimu wake? Huoni watunga sheria ambao ni waganga na waganguzi?
 
Mbona unahofu,kama ulikabidhiwa mikoba lako ilo.kama vitabu vya dini vinaongea juu ya uchawi nini katiba
 
nipe majina ya vigogo 10 wa ngazi za juu za chama na baraza la mawaziri ambao hawatumii ushirikina
 
Wakati wa kuelekea uandikwaji wa katiba mpya, katika karne ya 21 bado taifa linafikia wakati wa kutoa kibari kwa waganga wa kienyeji kupita ndani ya nyumba za watu kusaka uchawai na irizi, hii ni picha ya wazi jinsi taifa lilivyopoteza uelekeo na kutumia muda mwingi katika kupambana na uchawi badala ya kukuza uchumi.

Katika wilaya ya ilala kata ya ukonga serikali imetoa kibari kwa mganga wa kienyeji aitwaye manyaunyau kutafuta wachawi wote katika kata hii, je hivi ndivyo vipaombele vya serikali yetu?

kama hiv ndivyo vipaombele basi kwenye katiba mpya tuweke sheria ya uchawi na serikali ikubali matumizi yake na kuingiza katika nyenzo za serikali,

Uchawi upo hata biblia inakiri hilo,ila inaonekana unahofu sana wewe mchawi nini?
 
Huyo manyaunyau noma, atakuumbua hapo mtaani kwako. Nakushauri uondoe hizo bunduki zako(ndumba) hata kama bado zinapumua kama chura. Hautapungukiwa kitu. ACHA JAMAA AFANYE KAZI. Alitusaidia sana hapa mtaani kwetu. sasa tunalala kwa amani.
 
mchawi lazima amtambue mchawi mwenzie, kama serikali iko makini ingetumia watu wa MUNGU kuwatoa wachawi si manyaunyau, ACHENI IMANI HABA KWA MUNGU KILA JAMBO LINAWEZEKANA
 
Viongozi wa serikali wawatumia sana wakati wa uchaguzi,so wanaogopa wakiwatosa now itakula kwao wakati wa uchaguzi
 
Hivi ile kesi yake ya wizi kule Mwanza iliishaje? Au ameizima kwa kutumia ndumba zake? Na kuhusu serikali kuukubali uchawi tusisahau kuwa hata Rais wetu analindwa na majini,wale vijana wa PSU wanageresha tu sana sana labda kumdaka anapojiwa na ule ugonjwa wake wa kuanguka.
 
Wakati wa kuelekea uandikwaji wa katiba mpya, katika karne ya 21 bado taifa linafikia wakati wa kutoa kibari kwa waganga wa kienyeji kupita ndani ya nyumba za watu kusaka uchawai na irizi, hii ni picha ya wazi jinsi taifa lilivyopoteza uelekeo na kutumia muda mwingi katika kupambana na uchawi badala ya kukuza uchumi.

Katika wilaya ya ilala kata ya ukonga serikali imetoa kibari kwa mganga wa kienyeji aitwaye manyaunyau kutafuta wachawi wote katika kata hii, je hivi ndivyo vipaombele vya serikali yetu?

kama hiv ndivyo vipaombele basi kwenye katiba mpya tuweke sheria ya uchawi na serikali ikubali matumizi yake na kuingiza katika nyenzo za serikali,
Mhhh hii nayo ni siasa?
 
nadhani nimeona maoni ya wengi wengine wakisema kutoa habari hii humu ni hofu wengine wakisema ya kuwa viongozi wa serikali wameingia kwa njia hii.

lakini kikubwa si shughuli za mtu huyu bali kikubwa ni je nchi kutoa kibari kwa mtu huyu ni utawala wa sheria. Ingawa amepita katika madaraja na inasemekana ametoa irizi na mtoto aliyechukuliwa msukule kwenye daraja moja linaloenda mongolandege. lakini ni jambo linalotakiwa kujadiliwa na liwekwe sawa, je serikali zetu zinatakiwa kutoa vibari vya waganga wa kienyeji kupiga ramli wakati pinda alipinga na kusema ni vitendo vinavyochangia mauaji ya albino?
 
Back
Top Bottom