Manyara: Watoto wawili wamefariki kwa kula boga lenye sumu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
Watoto wawili wafariki kwa kula boga lenye sumu
Wilayani kiteto mkoani manyara, mmoja ni wa kiume umri miaka 8, wa pili ni wa kike mwenye miaka8, wawili walionusurika wakilazwa hospitalini.

Walionusurika wamepelekwa hospital ya rufaa Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto wamewatembelea Wagonjwa hospital na kuomba madaktari kufanya uchunguzi kujua ni aina gani ya Sumu na kuwaomba Wanannchi kuwa makini na vyakula wanavyokula. Na kama kuna mtu atavimba tumbo watoe taarifa mapema.
85d526f25d7a0e3feb97ec486c6ec62d.jpg

Waliopoteza maisha wametajwa kuwa ni Leiyoo Birikaa (6) na Nanyori Birikaa (12), wote wakazi wa Kijiji cha Partimbo, wakati waliolazwa hospitalini ni Kitwaini Birikaa (12) Orkiang Birikaa (7) na Taleck Birikaa (6)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom